Home Uncategorized WACHEZAJI SIMBA WAGOMA KISA MPUNGA

WACHEZAJI SIMBA WAGOMA KISA MPUNGA


Baada ya kikosi cha Simba (U20) kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Bara, imeelezwa kuwa wachezaji wa timu hiyo wamevunja kambi.

Kikosi cha vijana cha Simba kimevunja kambi kufuatia kutolipwa fedha zao za mahahara kwa muda wa miezi sita.

Taarifa imesema kuwa wachezaj takribani wote wa kikosi hicho wameondoka kuelekea makwao ikiwa ni kigezo cha wao kutolipwa na ikielezwa wamefanya hivyo ili kulipwa fedha zao.

Wakati wakiondoka na kukacha kambi, Simba B wanapaswa kucheza na Yanga B katika mchezo wa kuwania mshindi wa tatu.

Simba B wanakutana na Yanga B baada ya kutolewa na Mtibwa huku Yanga akitolewa na Azam kwa mikwaju ya penati.

SOMA NA HII  SAMATTA AUNGANA NA SERIKALI KUFANYA JAMBO LA KIHISTORIA