Home Uncategorized TAIFA STARS MUDA WA KUTUSUA NI SASA FANYENI KWELI

TAIFA STARS MUDA WA KUTUSUA NI SASA FANYENI KWELI

MWENDO wa hesabu kali Kwa sasa ukizingatia kwamba tumekwama kwa muda wa miaka 39 tukishuhudia wengine wakionyesha maajabu yao kwenye michuano mikubwa ya Afcon sasa nasi tumepenya kwenye tundu la sindano. 
Nafasi hii adimu inapaswa itumiwe kwa unyenyekevu wa kipekee hasa kwa wale ambao wamepewa dhamana ya kupeperusha Bendera ya Taifa letu kubwa Tanzania. 
Wachezaji ambao wamechaguliwa ni kazi yao kutimiza jukumu la Taifa kwani wameaminiwa na kukabidhiwa cheo kikubwa ambacho ni zaidi ya balozi wa nchi kwa muda ambao watakuwa nchini Misri kupambana.
Tumeona namna ambavyo wamewahi kuweka kambi mapema jambo litakalosaidia kuongeza morali ya kutafuta matokeo chanya kwani kikwazo cha ugeni wa mazingira kitakuwa si sehemu ya sababu za kufeli Kwa timu.
Pia benchi la ufundi limeongezewa nguvu ni jambo jema ambalo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamefanya kwa wakati muafaka wanastahili pongezi Kwa hilo.
Pongezi hizi kubwa hazitakuwa na maana kama benchi mlilolipa majukumu makubwa ya Taifa litashindwa kukidhi haja ambayo wengi tunatarajia haitapendeza kwa kila mpenda maendeleo ya Soka. 
Hivyo benchi la ufundi linapaswa kupambana kuleta matokeo chanya ambayo yatasaidia kuongeza hamasa na mwitikio kwa watanzania ambao wana Imani kubwa na wawakilishi wao kwenye michuano mikubwa inayotarajia kutimua vumbi leo 21 huko Misri.
Michezo ya kirafiki ambayo imechezwa mpaka sasa nina imani imetoa picha halisi ya kile ambacho vijana wamefundishwa na kuweka akilini mpaka sasa kabla ya michuano kuanza kutimua vumbi rasmi.
Pia inatoa fursa ya mwalimu Emmanuel Ammunike kutengeneza kikosi cha ushindi kitakachotoa burudani na raha kwa mashabiki wa Tanzania wote hivyo ni muhimu kuongeza zaidi umakini.
Kwa namna ambavyo kila mchezaji anajitoa inasaidia kuonyesha namna ambavyo vijana wameanza kuelewa mbinu na mipango ya mwalimu wao Kwa sasa.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya wenyeji Misri ambao wao walitumia wenyeji wao pamoja na uzoefu wa kushiriki michuano hiyo.
Ushindi wa bao 1-0 walioupata iwe chachu kwa wachezaji kuamini kwamba inawezekana ukashinda bao 1 na ukalilinda Mwanzo mwisho hivyo waige mbinu za ushindi na kujituma kulinda ushindi watakaoupata wakati wa mashindano.
Sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Zimbabwe inaleta picha mpya kwamba uwezo wa kufunga upo hivyo ni lazima tujipange kwenye kila idara.
Mashabiki wa Tanzania tusisahau kwamba jukumu la kuisapoti timu ni letu sote kama ambavyo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe ametuomba tuisapoti kwa hali na Mali.
Kuichangia timu ya Taifa ili ifanye vema ni uugwana na kitendo cha uzalendo tusijisahaulishe ni wakati wetu kuipa sapoti timu yetu ya Taifa Kwa sasa 
Muhimu Kwa wachezaji wasijisahau kwamba wapo na kazi ngumu ya kufanya wanapaswa washirikiane mwanzo mwisho katika michezo yote kupata matokeo na kuyalinda matokeo watakayoyapata.
Kwa wale wenye uwezo wa kwenda nchini Misri basi ni wakati muafaka sasa kukwea pipa kutoa sapoti kwa timu yetu ya Taifa huko walipo.
Wengi wanahofia gharama kuwa kubwa napenda kuwatoa hofu kwenye hilo kwani kuna makampuni ambayo yamejitoa kusimamia taratibu zote za usafiri.
Hivyo Kwa kufanya hivyo ni nafasi Kwa mashabiki kujiunga na timu ya Taifa nchini Misri kuwapa sapoti vijana wetu huko walipo kutaongeza joto la kujituma mwanzo mwisho.
Mashabiki ni muhimu Kwa ajili ya kuwapa moyo vijana kupambana uwanjani Ile amshaamsha za mashabiki zitaongeza nguvu Kwa wachezaji.
TFF pia inapaswa iangalie namna bora ya kuwapeleka mashabiki licha ya umbali wao wakiwa ni mabosi wa mpira kuna Jambo wanaweza kufanya Kwa ajili ya mashabiki hasa wale watakaopata nafasi ya kuibukia Misri 
Napenda kutoa rai kwa wachezaji kucheza Kwa juhudi isiyo ya kawaida ili kuonyesha kwamba miaka 39 imetupa funzo kubwa hivyo timu uwajibike kufuta maumivu yetu yote

SOMA NA HII  BALAA LA MZAMBIA ANAYEWINDWA NA SIMBA ACHA KABISA, DAU LAKE NOMA