Home Uncategorized IBRAHIM AME ATAMBULISHWA SIMBA, ASAINI MIAKA MIWILI

IBRAHIM AME ATAMBULISHWA SIMBA, ASAINI MIAKA MIWILI

 


IBRAHIM Ame beki aliyekuwa akikipiga Coastal Union leo Agosti 16 ametambulishwa ndani ya Klabu ya Simba.

Ame amesaini dili la miaka miwili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho Chenye maskani yake Msimbazi.

Anaungana na Pascal Wawa raia wa Ivory Coast mwili jumba kuimarisha safu ya ulinzi.

Pacha wake Bakari Nondo waliyekuwa pamoja naye Coastal Union yupo zake Yanga alikosaini dili la miaka miwili hivyo wamegawana mitaa, Nondo yupo Jangwani na Ame yupo Msimbazi

SOMA NA HII  BREAKING: YANGA WAKUTANA NA RUNGU LA TFF, KISA MASHABIKI UWANJA WA TAIFA