Home Habari za michezo YANGA WALAMBA SHAVU HILI KUTOKA NMB

YANGA WALAMBA SHAVU HILI KUTOKA NMB

Mwanachama wa Yanga akifungua akaunti atalipia Shilingi 34,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga (Shilingi 5,000 ni malipo ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 24,000 ni ada ya Mwanachama kwa mwaka mzima).

Mwanachama wa Yanga atalipia Shilingi 29,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga ambayo ni kadi ya Malipo ya kabla(Prepaid Card) shillingi 5,000 ni malipo ya kadi na shilingi 24,000 ni ada ya Mwanachama kwa mwaka mzima).

Kadi hizi hazitakua za uanachama/ushabiki tu, pia zina uwezo wa kufanya kazi kama kadi ya Benki! Unaweza kufanya miamala yote ya kibenki ikiwemo kuiwekea pesa, kutoa hela katika ATM na kufanya malipo mtandaoni na katika vituo vya malipo (POS).

Wanachama wanaweza kupata kadi za Malipo ya Kabla (Prepaid Card) ambayo huitaji kuwa na akaunti nasi na kufanya malipo kwa kupitia mtandao au kwenye Point of Sales (POS).

Wanachama wa Yanga watanufaika na huduma na ofa mbalimbali za NMB ikiwemo mikopo isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta) na punguzo la bei wakifanya malipo kupitia NMB Lipa Mkononi (QR).

Mbali na huduma za uanachama, NMB itaanzisha Bima ya Mwananchi ambayo itakua na gharama nafuu.

SOMA NA HII  IMBA AFUNGUKA HAYA JINI ZITAKAVYOBEBWA POINTI TATU MBELE YA WAARABU