Home Habari za michezo BAADA YA KOCHA MPYA WA YANGA KUTUA MASTAA HAWA KUPIGWA CHINI

BAADA YA KOCHA MPYA WA YANGA KUTUA MASTAA HAWA KUPIGWA CHINI

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga ametua juzi usiku kutoka Brazili, lakini kitu ambacho mashabiki wa klabu hiyo wanapaswa kukaa wakikujua mpema ni kwamba beki wa kulia, Djuma Shaban huenda akawa mchezaji wa kwanza kupiga panga ili kupisha jembe jipya kushuka Jangwani.

SOKA LA BONGO ilishawatarifu mapema kwamba Miguel Angel Gamondi ametua na faili zito la kufyeka baadhi ya mastaa waliosalia kikosini wakiwamo wakigeni na wale wazawa, lakini mtu wa kwanza ambaye anaweza kwenda na maji ni Djuma, beki mahiri kutoka DR Congo.

Beki huyo alisajiliwa kwa mbwembwe kubwa msimu miwili iliyopita akitokea AS Vita ya DR Congo, anatajwa ni mchezaji aliye kwenye rada ya kupitiwa na panga, kwani jina lake lilikuwapo tangu enzi za Kocha Nasreddine Nabi.

Nabi aliyeipa Yanga mataji saba yakiwamo mawili ya Ligi Kuu, mengine mawili ya ASFC na Ngao ya Jamii mara mbili pamoja na Kombe la Mapinduzi, inaelezwa alishatoa mapendekezo mapema juu ya wachezaji wa kuachwa kwa msimu ujao na majembe mapya ya kuingia kabla ya Gamondi kuajiriwa.

Hata hivyo mapema Gamondi aliuambia uongozi uzuie wachezaji kadhaa wasiondoke kikosini baada ya kupitia video ya mechi tano za mwisho za msimu uliopita zikiwamo mbili za fainali ya CAF, lakini baada ya kuchungulia tena video hizo amebaini kuna watu wa kutemwa tena.

Na kati ya wachezaji waliongia kwenye 18 za panga jipya, litakalotegemea na kocha Gamondi mara atakapokutana na mabosi wa klabu hiyo kuweka mambo sawa ni pamoja na Djuma.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kinasema kinchomponza Djuma ni kudaiwa ni mmoja kati ya wachezaji waliokuwa wakiendesha migomo ya chini chini klabu na kumchefua Nabi, huku mwingine akitajwa ni kiungo Yannick Bangala anayeweza pia kufyekwa na panga hilo jipya.

“Kuna asilimia kubwa kwa Djuma kwenda na maji, lakini tunasubiri kwamba kocha aje tumsikilize maamuzi yake, lakini jina jingine lililo kwenye hatari hiyo ni Bangala (Yannick), pia kuna wazawa kadhaa wanaoweza kupewa ‘thank you’ na kupelekwa kwa mikopo klabu nyingine,” kilisema chanzo hicho kilichofichua tayari jina la mrithi wa Djuma linaendelea kujadiliwa kwa sasa.

Kabla ya panga hilo lijalo, Yanga ilishawapa ‘thank you’, Dickson Ambundo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Erick Johora, Bernard Morrison na Tuisila Kisinda aliyerejesha klabu ya RS Berkane baada ya kuitumikia Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Yanga iliyokuwa Malawi ilipoenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimtaifa maalum dhidi ya Nyasa Bullets katika kuadhimisha Miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo, tayari imesharejea kabla ya kuitana kwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano ikianza na Ngao ya Jamii itakayopigwa Tanga.

Yanga ndio watetezi wa Ngao ya Jamii ikilishikilia kwa misimu miwili mfululizo kama ilivyo kwa Ligi Kuu Bara na Kombe la ASFC.

Safari Ngao itachezwa jijini Tanga ikishiri9kisha timu nne ikiwamo Azam, Simba na Singida Big Stars na watetezi Yanga baada ya Shirikisho la Soka (TFF) kufanya mabadiliko tofauti na ilivyokuwa awali ikishirikisha bingwa wa ligi na wa Kombe la ASFC.

SOMA NA HII  ISHU YA MAYELE KUONDOKA AU KUBAKIA YANGA IKO HIVI...AGOMEA MSHAHARA WA MIL 34 KWA MWEZI..