Home Habari za michezo IMBA AFUNGUKA HAYA JINI ZITAKAVYOBEBWA POINTI TATU MBELE YA WAARABU

IMBA AFUNGUKA HAYA JINI ZITAKAVYOBEBWA POINTI TATU MBELE YA WAARABU

Habari za Simba

IKIWA ni saa chache zimebaki kabla ya wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba kutupa kete ya tatu kusaka pointi tatu dhidi ya Wydad Casblanca wameweka wazi kuwa kwa nguvu ya Mungu watazipata pointi tatu.

Ipo wazi kwamba kwenye anga la kimataifa msimu wa 2023/24 mambo ni magumu kwa Simba katika mechi nne za Ligi ya Mabingwa hakuna ushindi zaidi ya kuambulia sare.

Ilikuwa Power Dynamos 2-2 Simba, Simba 1-1 Power Dynamos, Simba 1-1 Asec Mimosas na Jwaneng Galaxy 0-0 Simba leo utakuwa ni mchezo wa tano kwa Simba kimataifa.

Nyota wa Simba Fabrince Ngoma ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Wydad Casablanca utakuwa mgumu lakini watapambana kupata ushindi.

“Wachezaji tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa tunakutana na timu inayotafuta ushindi. Tupo tayari tunaamini kwa nguvu za Mungu tutashinda mchezo wetu na kupata pointi tatu.

“Kila mmoja anatambua kwamba huu ni mchezo muhimu kwetu na tunawaheshimu wapinzani wetu kutokana na uimara wao hilo tunalizingatia kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi,” .

Wydad kwenye mechi mbili hatua ya makundi haijashinda zaidi ya kupoteza huku Simba ikiambulia sare kwenye mechi zote hizo jambo linaloongeza ugumu kwenye mchezo wa leo.

SOMA NA HII  KUHUSU KIPOGO CHA SHABIKI WA YANGA, UONGOZI WACHUKUA MAAMUZI HAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here