Home Uncategorized ROSTAM APINGA YANGA KUMILIKIWA NA MTU MMOJA, ASISITIZA LUHUSU SUALA LA UDHAMINI...

ROSTAM APINGA YANGA KUMILIKIWA NA MTU MMOJA, ASISITIZA LUHUSU SUALA LA UDHAMINI SI UFADHILI


Mwanachama na shabiki maarufu wa klabu ya Yanga, Rostam Aziz leo ametokea hadharani na kusema kswamba haungi mkono klabu yake kumilikiwa na mtu mmoja.

Rostam ameyasema hayo leo mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo na waandishi, Rostam amesema hakubaliani na suala la mtu mmoja kumiliki klabu hiyo au kufadhili, badala yake anaunga mkono udhamini.

“Mtu mmoja amiliki klabu kubwa kama Yanga, yenye wanachama mamilioni. Hili si sahihi, hata ufadhili ni nia ya mango wa nyuma kuimiliki klabu,” alisema.

“Kwangu binafsi nitaendelea kuisaidia Yanga kama shabiki na mwanachama. Kikubwa ni uongozi kuangalia namna ya kufanya mambo yaliyo sahihi lakini si umiliki kutoka kwa mtu mmoja.

“Yanga inaweza kuingiza fedha zake kupitia udhamini, matangazo ya runinga lakini pia suala la kuuza bidhaa zake kama jezi na kadhalika,” alisisitiza.

SOMA NA HII  MOLINGA SASA KUONGEZEWA MKATABA YANGA