Home Uncategorized MGUNDA WA COASTAL UNION ATAJA IDADI YA WACHEZAJI ATAKAOWASAJILI

MGUNDA WA COASTAL UNION ATAJA IDADI YA WACHEZAJI ATAKAOWASAJILI


KOCHA wa timu ya Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kinahitaji kusajili wachezaji sita ambao wataongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Mgunda amesema kuwa ushindani msimu ujao utakuwa mkubwa tofauti na mwanzo hivyo ni lazima awe na kikosi makini kitakacholeta ushindani.

“Mpaka sasa bado mchakato wa usajili haujaanza ila hesabu ambazo zipo ni kuona kwamba tunasajili wachezaji sita ambao watakuja kuongeza nguvu pale ambapo kulikuwa na mapungufu kidogo msimu uliopita.

“Vijana wangu hawakuwa wazembe, wamepambana kufa na kupona ndio maaana tumebeki ndani ya ligi, msimu ujao ushindani utakuwa mgumu nasi tunapaswa tulete ushindani,” amesema Mgunda.


Coastal Union kwa msimu wa 2018/19 inashikilia rekodi ya timu iliyofungwa mabao mengi baada ya kukubali kufungwa mabao 8-1 na Simba uwanja wa Uhuru.

SOMA NA HII  ISMAEL RAGE AKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA, AACHIWA KWA DHAMANA