Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KUTEMWA….MORRISON NAYE AANZA KUJIBU...

SIKU CHACHE BAADA YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KUTEMWA….MORRISON NAYE AANZA KUJIBU MAPIGO KWA SIMBA…


Kiuongo wa Simba, Bernard Morrison raia wa Ghana ameondoa maelezo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo awali yalikuwa yakieleza kuwa ni mchezaji wa Simba Sc.

Ikumbukwe kuwa klabu yake ya Simba ilitangaza kuwa imempa mapumziko kwa ajili ya kwenda kushughulikia masuala yake binafsi ya kifamilia mchini kwao Ghana mpaka mwisho wa msimu pamoja na kumtakia kila la heri katika maisha yake ya soka yajayo.

Lakini Morrison ambaye mkataba wake na Simba unatamakika mwishoni mwa Juni, amekuwa akionekana katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa maana ya kwamba licha ya kupewa ruhusa ya kwenda kwao lakini hajaondoka mpaka sasa jambo ambalo linawafanya mashabiki na wadau wa soka wahisi huenda akatimkia kwa waajiri wake za zamani, Yanga.

SOMA NA HII  MAAFISA CAF KUTEMBELEA UWANJA WA MKAPA KUONA KAMA 'YALIYOMO YAMO AU LAAH'..FAINAL ITAPIGWA...