Home Habari za michezo HATIMAYE SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA YANGA…AHMEDI ALLY AKIRI MAMBO MAGUMU KWAO MSIMU...

HATIMAYE SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA YANGA…AHMEDI ALLY AKIRI MAMBO MAGUMU KWAO MSIMU HUU…

 


Klabu ya Simba imekiri kuwa mambo ni magumu na hakuna uwezekano wa kuwazidi kete watani wao Yanga katika mbio za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally katika mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza huku akitamba kuwa kwa kutambua hilo wameelekeza nguvu zote kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam ili kufuta machungu ya mambo magumu waliyoyapitia msimu huu.

Simba itavaana na Yanga Jumamosi katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa 9:30 alasiri.

Ally amesema kuchukua kombe hilo klabu itakuwa imetikimiza asilimia 70 ya malengo yake msimu huu baada ya mambo kuwaendea kombo Ligi Kuu.

“Maandalizi yanakwenda vizuri ni mchezo wetu wa maana na wa thamani kubwa unakwenda kufuta machungu tuliyopitia msimu huu.

“Ligi kuu mambo yanazidi kuwa magumu mpinzani wetu anazidi kulisogelea kombe lakini huku (Shirikisho) bado ni kweupe kuchukua taji hili tutakuwa tumetimiza asilimia 70 ya malengo yetu ya msimamo,” amesema Ally.

Amesema licha ya Yanga kujipambanua kuwa timu bora msimu huu lakini Wekundu wa Msimbazi kinaamini katika ubora wa kikosi chake kwani mechi za namna hiyo ndizo Simba anapenda kuzicheza huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuisaidia timu kutimiza malengo yake.

SOMA NA HII  GEITA GOLD WAKUTANA NA YA YANGA KWA SAIDO NTIBANZONKIZA...TFF WAONDOA JINA LAKE KWENYE MAJINA YA CAF....