Home Habari za michezo PAMOJA NA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA…’FYEKA FYEKA’ KUENDELA KURINDIMA SIMBA…

PAMOJA NA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA…’FYEKA FYEKA’ KUENDELA KURINDIMA SIMBA…

FT:Simba 1-0 Jamhuri

Klabu ya Simba SC imesema haijamaliza kuondoa wachezaji walioshuka viwango, au wote wasiojituma kwenye kikosi hicho na kutoa angalizo kuwa yeyote asiyefanya hivyo ataachwa mwishoni mwa msimu hata kama alisajiliwa kipindi cha dirisha dogo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’, amesema zoezi la kufyeka wachezaji wote wavivu, walioshuka viwango na wasiojituma bado linaendelea na linafanywa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha kwa kushirikiana na viongozi, hivyo kuwataka wachezaji wote waliopo sasa wafanye kazi ya kuipambania Simba SC na si vinginevyo.

“Dirisha kubwa linakuja, nasisitiza kusema tena huu tena si mjadala, hatutaangalia sura wala jina la mtu au wewe ni maarufu kiasi gani, au wapenzi wanakukubali kiasi gani, tunachotaka sisi ni kitu gani unatupa kwenye klabu yetu.

“Mchezaji umeajiriwa kazi yako ni kufanya kazi ya kuiletea ushindi Simba SC, ukishindwa tunakuondoa tunaweka mwingine kwa hiyo tutaendelea na panga hili kama kawaida, hivi sasa tunalinoa kwa ajili ya kufanya kazi mwishoni mwa msimu.

“Nitoe wito kwa wachezaji wote wafanye kazi ya kuisaidia klabu ya Simba SC, la sivyo ‘thank you’ itamhusu Mwishoni mwa ligi,” amesisitiza kiongozi huyo.

Tayari Simba SC imeshawatoa baadhi ya wachezaji na kuwapeleka wengine kwa mkopo mwishoni mwa dirisha dogo la usajili.

Wachezaji hao ni Jimmson Mwanuke na Nassor Kapama waliokwenda Mtibwa Sugar, Shaaban Chilunda akienda KMC, Jean Baleke aliyerejea TP Mazembe, na Moses Phiri ambaye ameeleka Power Dynamos ya Zambia.

Timu hiyo imewasajili Babacar Sarr kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Klabu ya US Monastir ya Tunisia, Salehe Karabaka kutoka JKU ya Zanzibar, Omar Jobe kutoka Zhenis ya Kazakhstan, Freddy Michael Kouablan, akisajiliwa kutoka Green Eagles ya Zambia, na Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar.

Try Again amesema Benchikha ndiye aliyependekeza wachezaji waliosajiliwa na walioachwa, huku wengine wakiponea kwenye Kombe la Mapinduzi.

AFCON 2023: Avram Grant achimba mkwara mzito
“Usajili huu ni mapendekezo ya mwalimu alitupa ripoti ya wachezaji wangapi tuwaache na wangapi tuwasajili na akatoa maelekezo ya maeneo ya kusajili na hata majina ya wachezaji akisema namtaka huyu.

Kwa hiyo niseme tu kuwa usajili wetu umezingatia maelekezo ya mwalimu na baadhi ya aliosema tuwaache wamekwenda kuponea Kombe la Mapinduzi, Zanzibar ambako baada ya kufanya vema akabadili msimamo wake na kuwabakisha kikosini,” amesema.

Ameongeza kuwa watakaojituma kwenye nusu msimu huu wataendelea kuwepo, lakini watakaoonekana wanacheza chini ya kiwango watawaondoa hata kama walisajiliwa kipindi cha dirisha dogo.

Awali, tuliwahi kusema kuwa mchezaji ambaye haonyeshi kiwango cha kujituma basi tutaachana naye, ndivyo itakavyokuwa na mwalimu wetu amebariki hilo, hata kama tulimsajili dirisha dogo ataondoka tu, msimu ujao tunataka kutengeneze kikosi cha wachezajl wenye uwezo mkubwa, wapambanaji na wenye nidhamu.” amesema Try Again.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUFUNGA SIMBA...KAGERE ASHINDWA KUJIZUAI..AFUNGUKA HALI HALISI...