Home Habari za michezo HII HAPA ‘LAST CHANCE’ KWA MASTAA HAWA SIMBA NA YANGA….WAKIZUNGUA WATASEPA KILAZIMA..

HII HAPA ‘LAST CHANCE’ KWA MASTAA HAWA SIMBA NA YANGA….WAKIZUNGUA WATASEPA KILAZIMA..

Habari za Michezo

LIGI Kuu Bara imesimama kwa muda kupisha Fainali za Afcon 2023 zinazoendelea Ivory Coast na michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo ilimalizika Januari 13 kwa Mlandege kubeba taji hilo. Ni kipindi michuano hiyo na ile ya Fainali za Afcon ikiendelea, kulikuwa na vita ya usajili kwa miamba ya Ligi Kuu Bara na wachezaji walikuwa wakipishana mlangoni kwenye vikosi huku wengine wakitoka kwa mkopo na majembe mapya yakishushwa.

Hata hivyo, wakati w3engi wakiendelea na burudani za Mapinduzi na Afcon zinazoendelea Ivory Coast, kuna baadhi ya wachezaji walikuwa matumbo joto wakitafakari hatima zao, kama wanasalia au wanaachwa na timu zao kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15 msimu huu wa 2023/2024.

Wapo walioachwa na kwa sasa hawana timu, wengine wameuzwa na kutolewa kwa mkopo na wale walioondoklewa kabisa kwenye orodha ya usajili na sasa wanasikilizia michongo, hata hivyo, Mwanaspoti linakuletea wachezaji wa timu tatu za juu kwenye msimamo wa ligi kwa maana ya Azam, Yanga na Simba ambao walinusurika kuachwa kwenye dirisha hilo na sasa ni nafasi yao ya mwisho kuonyesha ubora wao ili kuepuka mkono wa kwa heri mwisho wa msimu.

LUIS MIQUISSONE
Alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba. Akatengeneza ufalme wake. Bao lake la ufundi alilowatungua Al Ahly likasababisha kuondoka kwenye timu hiyo na kwenda Misri. Al Ahly walivutiwa naye na kumwekea dau nono mezani na kuinasa saini yake.
Hata hivyo, kuondoka kwake Simba kulisababisha nafasi yake kupwaya na kila aliyepita kwenye kikosi hicho hawakuweza kuziba pengo lake.

Al Ahly mambo hayakuwa mazuri na hiyo iliwafurahisha Simba walioamini na kumwimba kijana wao arudishwe nyumbani na viongozi hawakufanya ajizi, Luis akarudi Msimbazi.

Hata hivyo, tangu amerudi Msimbazi hajawa na kiwango bora kama ilivyotarajiwa na hadi sasa katika mechi 10 za Simba kwenye Ligi Kuu amehusika na mabao matatu tu akitoa asisti na hana bao.

Mara kwa mara amekuwa akikosa nafasi kikosi cha kwanza kutokana na kuanza kinyonge na kulikuwa na tetesi huenda akaachwa dirisha dogo lililopita lakini ameendelea kusalia kikosini. Huu ni wakati sasa wa kuonyesha alistahili kubaki la sivyo mwisho wa msimu anaweza kuagwa Msimbazi.

SAID NTIBAZONKIZA
Fundi wa mpira. Namba hazidanganyi. Inaelezwa tangu akiwa na majirani zao, Yanga, Simba ilikuwa ikimtamani. Hata hivyo aliondoka Jangwani na kurudi kwao Burundi kabla ya kutua Geita Gold na kukiwasha kinoma.

Hilo lilizidisha hamu ya Simba kuinasa huduma yake na fasta wakamvutia waya. Akiwa Geita alionyesha kiwango bora na Simba ikamsajili na msimu uliopita alimaliza kinara wa mabao sambamba na Fiston Mayele wakifunga mabao 17 kila mmoja.

Hata hivyo, msimu huu hajawa na kiwango bora kama alivyoonyesha msimu uliopita na hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara mechi 10 za Simba amefunga mabao manne na kusababisha mashabiki wa timu hiyo kumwimba amezeeka na anatakiwa kupisha damu changa.

Kiungo huyo mshambuliaji alikuwa ni mmoja wa nyota waliotajwa ataachwa dirisha dogo la usajili lililopit, lakini ameendelea kusalia kikiosini na hasa baada ya Kocha mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha kuuomba uongozi kumwongeze mkataba kutokana na aina yake ya uchezaji, pia ni mchezaji anayeelewa lugha nyingi hivyo ni msaada wa mawasiliano kwenye timu. Hata hivyo, kusalia kikosini ni mtego kwake na akishindwa kufanya vizuri hadi mwisho wa msimu, panga litamuhusu.

GIFT FREDY
Haimbwi sana. Ana uwezo, lakini Yanga kuna watu wa nguvu wanaosababsha asugue benchi. Gift wengi waliamini jina lake litakatwa dirisha dogo la usajili lililopita, lakini ghafla mambo yakabadilika. Amebaki.
Kwenye michuano ya Mapinduzi kwa baadhi ya mechi alizcheza, alionyesha kiwango kizuri na kudhihirisha licha ya kukosa nafasi mbele ya nahodha Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ wote wazawa, ana kitu.

Kiwango bora alichoonyesha Mapinduzi na huku dirisha la usajili likiendelea, kilisababisha kuwavuruga benchi la ufundi na viongozi wa Yanga na beki huyo raia wa Uganda ataendelea kuwepo lakini hiyo ikiwa ni mtihani kwake wa kuonyesha uwezo ili kukwepa shoka mwisho wa msimu.

DENIS NKANE
Hadi sasa hana uhakika wa kupata muda wa kucheza chini ya Miguel Gamondi tofauti na msimu uliopita alicheza mara kwa mara chini ya Nasreddine Nabi aliyekuwa akifanya mabadiliko ya wachezaji mara nyingi.
Tangu kutua kwa Gamondi, Nkane anayecheza winga amepoteza namba hadi kufikia hatua ya kutajwa ni miongoni mwa wachezaji watakaotolewa kwa mkopo, lakini mambo yamepinduka na ameendelea kubaki kikosini huku akisubiriwa kuona nini atafanya katika mechi zilizobaki msimu huu.

CLATOUS CHAMA

Kutoka kuwa kipenzi cha mashabiki, benchi la ufundi na viongozi hadi kuchukiwa na wengi ndani ya timu hiyo kutokana na kile kinachodaiwa ni nidhamu mbovu iliyosababisha asimamishwe kikosini hapo na kiwango chake kuporomoka ghafla tofauti.
Staa huyo alikuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba ambacho kilikuwa kikikosa huduma yake timu inayumba, lakini sasa hata asipokuwepo hakuna kinachoharibika hii ni kutokana na namna ambavyo mambo yamebadilika.

Chama ameondolewa kwenye orodha ya mastaa ambao wanaaminiwa na kupendwa zaidi tangu alipotua Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ambaye alimkataa muda mchache baada ya kukaa na timu na mashabiki kumjia juu, sasa wanamuunga mkono kwani hata kocha aliyepo Abdelhak Benchikha amekuwa akimpa muda mchache wa kucheza na inaelezwa kilichozuia kumwondoa kikosini ni aina ya mkataba alionao, hivyo wanasubiri dirisha kubwa na huenda wakaachana naye.

JAMES AKAMINKO
Jina lake lilitajwa sana aliposajiliwa na Azam FC na kuonyesha ufundi mkubwa bila kujali anakutana na mpinzani gani. Alipokutana na Yanga na Simba alionyesha ni fundi wa kuchezea mpira.

Aliimbwa sana hadi kufikia kipindi Simba na Yanga kuingia kwenye vita ya kutaka kunasa saini yake lakini sasa ghafla nyota yake imezima kuanzia kwenye timu yake hadi wale waliokuwa wanamuimba.
Ni miongoni mwa majina yaliyokuwa yanatajwa kuondolewa kwenye kikosi cha Azam FC huku mambo yakienda mbali zaidi hatakiwi na kocha, lakini cha ajabu dirisha limefungwa na staa huyo bado anaendelea kuitumikia timu hiyo na huu ndio muda wa kurejesha imani kwa mashabiki, uongozi na benchi la ufundi.

MAHALATSE MAKUDUBELA ‘Skudu’
Winga huyu machachari kutoka Afrika Kusini aliingia kikaangoni jina lake kujadiliwa ili kupunguzwa dirisha dogo la usajili lilopita, lakini amefanikiwa kupenya na kusalia Jangwani.

Skudu alitua Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Marumo Gallants baada ya kuwasumbua uwanjani kwenye mechi za Kombe la Shirikisho Afrika na kuamua kumsajili lakini tangu amevaa jezi za Wananchi mambo hayajamwendea vyema jambo lililoifanya Yanga kufikiria kumwondoa na kusajili winga mwingine lakini ghafla wakabadili mawazo na sasa amesalia ikiwa ni muda wake wa kufanya kile alichoonyesha akiwa Marumo.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUITWA TENA TAIFA STARS...ABDI BANDA AWARUSHIA MASTAA WENZAKE UJUMBE HUU 'LIVE'...