Home Uncategorized GWAMBINA FC KUKIWASHA LEO DHIDI YA YANGA

GWAMBINA FC KUKIWASHA LEO DHIDI YA YANGA

 


TIMU ya Yanga inashuka uwanjani leo Novemba 3, 2020  kuivaa Gwambina  katika mchezo wa kusaka kujiamini zaidi kwa mchezo ujao dhidi ya watani zao, Simba.

 

Usindi wa Yanga leo  katika Uwanja wa Gwambia utaifanya timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa raha zaidi licha ya sare pia inaweza kuwapa uongozi hadi matokeo ya Azam FC dhidi ya Dodoma Jiji.

 

Wageni hao wa Ligi Kuu, Gwambina watatakiwa kuwa makini na nyota wa kigeni wa Yanga, ambao wameonyesha kuwa mwiba mkali katika kufumania nyavu, kwani ni kipa pekee, Farouk Shikalo, ambaye hajafunga.

SOMA NA HII  RUVU YAKOMAA KUBAKI TP, MATOKEO NA TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA HAYA HAPA