Home news PAMOJA NA KUTUPWA NNJE LIGI YA MABINGWA…SIMBA YAPATA ZALI KIMATAIFA…

PAMOJA NA KUTUPWA NNJE LIGI YA MABINGWA…SIMBA YAPATA ZALI KIMATAIFA…


KAMA zali mwanangu. Simba imewekwa kwenye chungu Namba Moja kati ya vyungu vinne vya droo ya hatua ya mwisho ya mchujo ya Kombe la Shirikisho Afrika inayochezeshwa leo saa 8 mchana huko Cairo, Misri na la habari njema ni kwamba wapinzani wao wote wanafungika. Yaani yeyote aje.

Katika droo hiyo, timu 16 ambazo zimetolewa Ligi ya Mabingwa Afrika zitakutanishwa na zile zilizopenya hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kupata timu 16 ambazo zitaingia hatua ya makundi.

Timu 32 zimegawanywa katika vyungu vinne vyenye timu nane kila kimoja na timu za Chungu Na1. zitazikabili timu za Chungu Na.2 wakati timu za Chungu Na.3 zitakabili timu kutoka Chungu Na.4. Timu hizo nane ambazo Simba inaweza kutokuwa na presha kubwa ikiwa itapangiwa kutokana na historia na rekodi zao za hivi karibuni ni Marumo Gallants (Afrika Kusini), Coton Sports (Cameroon), Red Arrows (Zambia), DC Motema Pembe (DR Congo), Binga FC (Mali), Al Ahli Tripoli (Libya), Gor Mahia ya Kenya na JS Saoura ya Algeria.

Katika kundi hilo la timu nane, Gor Mahia ya Kenya ambayo kwa hivi karibuni imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiuchumi, ndio imeonekana kupata mafanikio makubwa zaidi katika mashindano ya klabu Afrika ambayo ni kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2018 na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo msimu wa 2018/2019.

Wengine ni JS Saoura ya Algeria ambao walitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/2019 ambapo walimaliza wakiwa mkiani mwa kundi D.

Mafanikio makubwa ya Al Ahli Tripoli ya Libya ni kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2017 na hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka 2016 na baada ya hapo haijatamba tena kimataifa.

DC Motema Pembe licha ya kuwahi kutwaa Kombe la Washindi Afrika mwaka 1994, haijapata tena mafanikio makubwa katika mashindano ya klabu Afrika wakati Coton Sport ya Cameroon inajivunia mafanikio yake ya kumaliza nafasi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008 na kumaliza katika nafasi hiyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika 2003.

SOMA NA HII  HATMA YA SIMBA IPO KWA MKAPA UONGOZI WAFUNGUKA HAYA KUHUSU WYDAD

Ukiondoa hizo, timu za Red Arrows, Binga na Marumo Gallants hazijawahi hata kufika hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika, iwe Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumzia kibarua kilicho mbele ya Simba kwenye Kombe la Shirikisho, Mwenyekiti wa Chama cha makocha Mwanza, Kessy Mziray alisema ana imani watafanya vizuri kwenye mashindano hayo ikiwa watajisahihisha makosa ya mechi iliyopita.

“Kwanza wanapaswa viongozi watambue huu ni mpira lazima wakubali matokeo, wamefanya makosa yamewagharimu kuhusu kufuzu hatua inayofuata ni viongozi benchi la ufundi wachezaji wanapashwa kuwa wamoja.”