Home news KUHUSU KIWANGO CHA SIMBA MSIMU HUU…VICTOR COSTA AIBUKA NA HILI…ADAI KUNA KITU...

KUHUSU KIWANGO CHA SIMBA MSIMU HUU…VICTOR COSTA AIBUKA NA HILI…ADAI KUNA KITU KIMEJIFICHA…


BEKI kisiki wa zamani wa Simba, Victor Coasta ‘Nyumba’ amesema licha ya mastraika wa kikosi hicho kuigharimu timu hiyo kwa sasa, lakini anaamini kuna jambo lingine la zaidi nyuma ya pazia ndani ya klabu hiyo kongwe nchini.

Simba imewashtua mashabiki wake, baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila kupata ushindi, ikipasuka mara mbili na kuambulia suluhu moja, huku katika mechi yao ya mwisho Kocha Pablo Franco aliwapiga chini mastraika wake wote.

Costa alisema Simba inacheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi, ila imeshindwa kutumbukiza mpira nyavuni jambo alilomshauri Pablo kulifanyia kazi mapema.

Beki huyo haungi mkono kitendo cha kocha kubadili badili kikosi kila mara kwani jambo hilo linasababisha timu hiyo kutotulia na kushindwa kutimiza malengo yake uwanjani na kuongeza; “Nikingalia Simba kwa sasa nahisi kuna kitu ndani ya timu, haiwezekani mastraika watatu waliongoza msimu uliopita waliongoza kwa mabao mengi ndani ya timu na Ligi nzima leo washuke kiwango ghafla.”

Beki huyo aliyewahi kuibuka Yanga kwa saa kadhaa kabla ya kurejea Msimbazi mwaka 2005 alisisitiza;

“Kuna kitu kimejificha, viongozi wamalize hilo haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi la sivyo kwa sasa kila mchezaji Simba ataonekana hafai.”

Kauli ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Abdallah Salim “Try Again’ naye alikiri kuwa hali wanayopitia sio kawaida, ila anaamini mambo yatabadilika ili Simba kurejea kwenye makali yake na kuwapa raha mashabiki.

SOMA NA HII  KUHUSU KASHFA ZA KUHUJUMU SIMBA...MATOLA AVUNJA UKIMYA...AANIKA A-Z MSIMAMO WAKE...