Home Habari za michezo NABI:SIJAWAHI KUFUNGIWA WALA KUPEWA ADHABU ZAIDI YA HAPA TANZANIA…NIMEONEWA SANA..

NABI:SIJAWAHI KUFUNGIWA WALA KUPEWA ADHABU ZAIDI YA HAPA TANZANIA…NIMEONEWA SANA..

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema katika nchi ambazo amefundisha soka hakuwahi kukumbana na adhabu ya kadi nyekundu wala kufungiwa mechi tofauti na ilivyo Tanzania.

Nabi amesema hayo leo wakati akizungumza kuhusu kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kumfungia mechi 3 na faini ya sh 500, 000.

TPLB imesema Nabi amefungiwa kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na mwamuzi wa akiba wakati wa mchezo kati ya Ihefu na Yanga kwenye wa Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya Novemba 29.

Nabi amesema alichokifanya wakati wa mchezo huo ni kumtaka mwamuzi wa mchezo huo kuchezesha kwa kufuata sheria na siyo kupendelea upande mmoja.

“Sina budi kukubali maamuzi ya kamati lakini ni kama imenionea sababu mazungumzo yangu yalikuwa ya kujenga na siyo malumbano kama ambavyo imeelezwa kwenye taarifa hiyo,” amesema Nabi.

Hiyo ni mara ya pili kwa Nabi kufungiwa ambapo msimu uliopita alifungiwa mechi tatu kutokana na kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Raphael Ikambi katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA dhidi ya Geita Gold.

Klabu alizofundisha kocha Nasreddine Nabi kabla ya kujiunga na Yanga ni AC Leopard ya Congo, DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Al Hilal na El Merreikh za Sudan, Ismaily ya Misri, AL Ahly Benghazi ya Libya na PDH ya serie D ya Italia.

Yanga ilimtangaza Nabi kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Aprili 20, 2021.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUJAA MASTAA WA KAZI KAZI...YACOUBA SOGNE ACHONGEWA MCHONGO WA KUTUA GEITA GOLD...