Home Uncategorized CIOABA KWENYE MTIHANI MZITO MNDANI YA BONGO, JUMATANO

CIOABA KWENYE MTIHANI MZITO MNDANI YA BONGO, JUMATANO


ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC, Jumatano ana kibarua kizito mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00.

Azam FC imetoka kushinda mchezo wao mbele ya JKT Tanzania kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Anderw Simchimba wakiwa ugenini Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mchezo wa kwanza uliowakutanisha wapinzani hao Simba ilishinda bao 1-0 na lilifungwa na Meddie Kagere mwenye mabao 14 kwa sasa ndani ya ligi.

Simchimba amesema kuwa kila baada ya kumaliza mchezo wamekuwa wakiangalia makosa yao na kujipanga kwa ajili ya mechi inayofuata.


SOMA NA HII  KAGERE ATAJA KINACHOMBEBA NDANI YA SIMBA