Home Uncategorized USHNDI WA MABAO 2-0 MBELE YA NDANDA YAIPA JEURI MTIBWA SUGAR

USHNDI WA MABAO 2-0 MBELE YA NDANDA YAIPA JEURI MTIBWA SUGAR

OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa sasa klabu hiyo imerejea kwenye ubora baada ya kushinda mabao 2-0 mbele ya Ndanda mchezo uliochezwa Uwanja wa Gairo, Februari 29.

Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Juma Liuzio dakika ya 11 kwa pasi ya Riphat Khamis na bao la pili lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 85.

Kifaru amesema: “Hatukuwa kwenye mwendo mzuri hasa kwenye mechi zetu saba za nyuma kwa kuwa tumeanza kushinda tunarejea kwenye kasi yetu na mambo mazuri yanakuja mashabiki watupe sapoti.

“Wakata miwa kwa sasa tumezinduka na tutaendeleza vita ya kusaka pointi tatu kwenye mechi zetu zote,” amesema.

Mechi inayofuata kwa Mtibwa Sugar itakuwa Jumatano, Uwanja wa Gairo dhidi ya Namungo FC ya Lindi.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED KUMALIZANA NA JKT TANZANIA LEO