Home news NIYONZIMA NA YANGA MPAKA MAKUNDI CAF

NIYONZIMA NA YANGA MPAKA MAKUNDI CAF

Habari za Yanga

Aliyekuwa kiungo wa Simba SC na Young Africans, Haruna Niyonzima ameutazama moto wa Young Africans mpya chini ya Muargentina, Miguel Gamondi na kutamka kuwa ana uhakika Al Merrikh hawatoki hivyo wajiandae kwa kipigo Rwanda.

Niyonzima alizichezea kwa mafanikio makubwa Simba SC na Young Africans katika vipindi tofauti na kuwa miongoni mwa mastaa wa kigeni ambao wamefanikiwa kupata mafanikio makubwa akishinda Kombe la Ligi Kuu Bara mara tano mfululizo na kuipeleka Simba SC Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.

Nyota huyo kwa sasa yupo kwao nchini Rwanda ambapo ameweka wazi kuwa anawakaribisha Young Africans huku akiwaahidi kutoa ushirikiano kwa timu hiyo katika mchezo wao.

Niyonzima amesema kuwa amefurahi kuona ndugu zake wa Young Africans wakiwa wanakwenda kucheza Rwanda katika taifa lake dhidi ya Al Merreikh.

“Nimewaangalia Young Africans ya msimu huu na naweza kusema wala wasiwe na wasiwasi wa kupata matokeo, kwa ubora wa kikosi chao ni wazi wao wana nafasi nzuri ya kusonga mbele kwa kuwa wana timu imara na bora zaidi ya wapinzani wao.”

“Al Merreikh ni timu bora lakini kwa kipindi hiki Young Africans ni bora zaidi, kwenye upande wa historia wapinzani wapo vizuri ila kwenye ubora wa wakati huu, Young Africans wapo vyema zaidi na naamini watapenya na kupata matokeo mazuri,” amesema Niyonzima.

Katika hatua nyingine Afisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe amesema kuwa malengo makubwa ni kufanya vizuri katika mashindano yote na kwenye Ligi ya Mabingwa Afika wanahitaji kupata matokeo ikiwa ni pamoja na mechi yao dhidi ya Al Mereikh.

Mechi zetu zote ni muhimu ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri, tunaamini kila kitu kitakwenda sawa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi katika mechi zetu zote.

“Katika ligi ya mabingwa Afrika malengo yetu msimu huuni kufika katika hatua ya makundi. ili tupate hiyo nafasi ni mnuhimu kuanza kufanya vizuri kwenye mechi hizi za mwanzo,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  M-Bet YAWAPA MAMILIONI MASHABIKI YANGA WALIOSHINDA