Home news M-Bet YAWAPA MAMILIONI MASHABIKI YANGA WALIOSHINDA

M-Bet YAWAPA MAMILIONI MASHABIKI YANGA WALIOSHINDA

 


MASHABIKI wawili wa mpira wa miguu wamejishindia  jumla ya Sh 85,996, 360 baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya michezo 12 ya mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.

Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi aliwataja washindi hao kuwa ni Dominic Mdimi ambaye anashabikia Klabu ya Yanga ambapo amefanikiwa kushinda kwa mara ya pili droo ya Perfect 12. Mdimi alishinda mara ya kwanza Oktoba 2019 Sh 36 millioni.

Mushi alimtaja mshindi mwingine ni Valentino Ngole wa Njombe  ambaye ameshinda kwa mara ya kwanza katika kushinda droo hiyo. Ngole pia ni shabiki wa Yanga.

Amesema kuwa Mdimi na Valentino wanakuwa washindi wa saba tangu kuanza kwa mwaka huu na kuendelea kuwainua vipato watanzania.

“M-Bet Tanzania itaendelea kuwa nyuma ya mabingwa na mpaka sasa tuna washindi watano ambao wameibuka kuwa mamilionea kupitia michezo yao,” amesema.

Kwa upande wake, Mdimi amesema kuwa ushindi wake umetokana na kuwa makini katika kuchagua timu bila ya kufuata alama za ushindi ambazo kilatimu imekuwa ikipewa katika mkeka.

Amesema kuwa pamoja na ushindi bado Klabu ya Arsenal inampa changamoto sana, hata hivyo, safari hii haikuwepo katika mkeka ambao yeye alibashiri.

“Siri kubwa ya kushinda bahati nasibu hii kujua uwezo wa timu pamoja na kufanyia utafiti wa timu, aina ya wachezaji ambao wamesajili, aina ya timu unayocheza nayo pamoja na majeruhi,” amesema Mdimi.

Ngole amesema kuwa amefarijika sana na ushindi kwani utamfanya kufungua biashara ili kujiongezea kipato.

“Nilikuwa nabashiri na kupata fedha kidogo kama Sh 200,000 na fedha nyingine kidogo, sijakata tamaa na sasa kufanikiwa kupata fedha ambazo nitafanyia masuala ya maendeleo,” amesema Ngole.
SOMA NA HII  BAADA YA KUPEWA 'UKOCHA MKUU' KWA MUDA....HIZO TAMBO ZA MATOLA KWA MBEYA CITY UTAFIKIRI MOURINHO AISEE...