Home Habari za michezo NAMBA 6 WA YANGA, BEKI AFUNGUKA BALAA LAKE

NAMBA 6 WA YANGA, BEKI AFUNGUKA BALAA LAKE

Mara baada Yanga kumtambulisha nyota wa Marumo Gallants, Mahlatse Makudubela, beki aliyekuwa akicheza naye, Mpho Mvelase ameeleza jinsi Yanga watakuwa wamelamba dume kutokana na ubora wake.

Skudu amepewa jezi namba 6 ambayo iliachwa wazi na kiungo wa zamani wa Yanga Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyeuzwa Azam FC.

Mpho ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wanaocheza kikosi cha kwanza cha Marumo, amesema Yanga kumsajili winga huyo ni jambo bora kwani ana uzoefu mzuri utakaowasaidia hasa katika michuano ya kimataifa kwa kuwa ana kasi, uwezo wa kupiga pasi zinazofika, pia ni mzuri katika kuimarisha ulinzi.

Aidha amesema ukiachana na suala la umri kuwa ni mkubwa, bado kwake siyo kikwazo kwani anachofahamu timu kubwa kama Yanga kwa sasa inahitaji wachezaji wenye uzoefu ambao watafanya vizuri hasa kimataifa.

“Uwezo wake wa kupambana akiwa uwanjani ni mkubwa sana lakini bila kusahau mbinu na uzoefu alionao ndio uliowavutia zaidi Yanga kumchukua, hivyo umri sio kikwazo kwani hata waliohitaji huduma yake hilo walilifahamu.”

“Yanga hawatajutia kuwa naye, sisemi kwa sababu nimecheza naye ila kizuri kinajiuza na kuonekana na nina uhakika atafanya makubwa msimu ujao kwani ni mtu anayejua nini anachokitaka kama mchezaji, ni mzuri wa pasi za mwisho, krosi na hata kwenye eneo la ulinzi anaweza kuwapa msaada mkubwa,” alisema staa huyo.

Mbali na Marumo staa huyo pia amewahi kuzichezea timu za Afrika Kusini, Chippa United na Orlando Pirates kwa mafanikio makubwa, anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu sana kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini.

SOMA NA HII  RASMI...AZAM FC WAZIDI KUTIA MACHUNGU SIMBA SC...WAMALIZANA NA SOPU KWA DAU NONO...ALAMBISHWA MIAKA MITATU...