Home Habari za michezo CAF WANASUBIRI USAJILI WA YANGA KIMATAIFA, TFF YATOA NENO

CAF WANASUBIRI USAJILI WA YANGA KIMATAIFA, TFF YATOA NENO

YANGA YATOA SIRI NZITO USAJILI WA MUSONDA...ULE NI USAJILI WA KIMKAKATI

Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limethibitisha kuwa Klabu ya Young Africans hadi sasa haijafanya usajili wa Michuano ya Kimataifa (Ligi ya Mabingwa Barani Afrika) msimu ujao 2023/24, hadi sasa.

Mapema leo Alhamis (Julai 20) TFF imetoa taarifa hiyo kupitia vyanzo vyake vya habari, huku Klabu nyingine zitakazoshiriki Kimataifa msimu ujao zikifanya usajili ambao umeshatambuliwa na CAF.

Taarifa hiyo inaonesha hadi sasa Azam FC, Singida Fountain Gate na Simba SC ndizo zimefanya usajili wa Kimataifa ambao unatambuliwa na CAF kupitia TFF.

Tariq Simba aomba ushirikiano Geita Gold
Hata hivyo hadi sasa haijafahamika kwanini Young Africans haijawasilisha CAF majina ya wachezaji iliowasajili, licha ya kuonekana wakiendelea kuwatambulisha wachezaji ambao wamesajiliwa katika kipindi hiki.

Caf

Ikumbukwe kuwa Young Africans ambayo ni Bingwa wa Tanzania Bara itashiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika sambamba na Simba SC, huku Azam FC na Singida Fountain Gate zikitarajia kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao 2023/24.

SOMA NA HII  WACHEZAJI HAWA WALIOACHWA NA SIMBA, YANGA WAPATA MAJANGA KATIKA USAJILI