Home Habari za michezo UNAAMBIWA YANGA WAMEKUTANA NA KIBONDE……ISHU IKO HIVI

UNAAMBIWA YANGA WAMEKUTANA NA KIBONDE……ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

Mchambuzi wa TV3 Alex, Ngereza amedai kuwa timu ya soka ya Yanga SC imekuwa kikikutana na vibonde kwenye mashindano ya CAF ndiyo maana inashinda kirahisi na kufanya kufanya vizuri.

Ngereza amesema hayo mara baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa katika Dimba la Kigali Pele, Rwanda jana Jumamosi.

Kabla ya mchezo huo, Yanga ilikutana na ASAS FC ya Djibouti ya kuifunga jumla ya bao 7-1 katika michezo miwili.

Ikumbukwe pia kuwa Msimu uliopita Yanga iliifunga Zalan FC ya Sudan Kusini mabao 9 kwenye michezo miwili kabla ya kutolewa na Al Hilal na kuangukia Kombe la Shirikisho ambapo Yanga ilicheza mpaka hatua ya fainali.

“Yanga wana bahati ya kukutana na Vibonde tangu msimu uliopita kwenye kombe la shirikisho barani Africa na msimu huu kwenye club bingwa barani Africa kwenye hizi hatua za awali

“El Merrick wamechoka kiaina kwahio Yanga wasijisifie sana tusubiri kwenye hatua ya makundi ndio wataenda kukutana na timu bora zenye wachezaji bora kama wao ndio tutaona kweli yaliomo yamo au itakuwaje,” amesema Alex Ngereza.

SOMA NA HII  ORODHA YA WACHEZAJI WA SIMBA WALIOANZA MAZOEZI LEO BOKO