Home Habari za michezo BAADA YA KUONJA UTAMU WA SIMBA….MOSES PHIRI AVUNJA UKIMYA ANAYOYAONA KAMBI YA...

BAADA YA KUONJA UTAMU WA SIMBA….MOSES PHIRI AVUNJA UKIMYA ANAYOYAONA KAMBI YA MISRI…


Kikosi cha Simba kimetimiza muda wa wiki moja kambini nchini Misri, ikijiandaa na msimu mpya wa mashindano, huku nyota wake wa kigeni, Moses Phiri na Hennock Inonga wakitamba kwa mziki uliopo Msimbazi, wapinzani wakizubaa watapigwa nyingi uwanjani.

Kocha Zoran Maki aliyewatengeneza ratiba moja matata ambayo imewafanya mastaa waliopo kwa sasa kambini humo kuichekelea, huku wakitamba wakitoka hapo watakuwa wameiva kisawasawa.

Phiri na Inonga waliotua kambini siku chache baada ya wenzao 19 kutangulia, walisema kwa nyakati tofauti kuwa mambo ni freshi sana.

Phiri aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Zanaco ya Zambia alisema amefurahia maandalizi kuanza mapema akiamini inatoa muda mzuri kwa wachezaji kuzoeana na wakitoka huko watakuwa moto kwa vile asilimia kubwa wamekutana wenye vipaji, uwezo nma uzoefu mkubwa wa mashindano mbalimbali.

“Uzuri wake naamini wachezaji wengi mbali ya kutoka mapumziko, lakini walijiweka vyema ndio maana imekuwa rahisi kwao kujifua bila tatizo. Kwa kipindi hichi cha pre-season kama wachezaji tutafanya vizuri maana yake tutakuwa moto na kuisaidia timu katika michuano shiriki,” alisema Phiri.

Mshambuliaji huyo anayesifika kwa kasi, nguvu, chenga na uwezo mkubwa wa kufunga alieleza imani yake juu ya kikosi cha Simba na kuweka wazi watakapomaliza kambi timu itatisha.

“Tuna timu nzuri, tunatumia pre-season hii kujijenga zaidi na kuzoeana sambamba na kuzielewa mbinu na mifumo ya kocha mpya hivyo tukirudi Tanzania tutakuwa tayari kupambana na kushinda vita yeyote,” alisema Phiri na kuongeza;

“Timu yetu imejengeka zaidi msimu huu benchi la ufundi limefanyiwa maboresho, wachezaji wapya tuliyoingia kwa kushirikiana na waliokuwepo msimu uliyopita naimani kubwa tutafanya vizuri.”

Inonga aliyekuwa kikosi kilichopita na kushinda tuzo ya Beki Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, alisema; “Msimu uliopita hatukuwa vibaya, lakini hatukufanya vizuri kama tulivyotarajia.

Muda huu tunajiandaa ili kufanya vizuri msimu ujao, kila mchezaji aliumizwa na kushindwa kutwaa makombe na sasa tuaedelea kujipanga turudi kwa kishindo na wapinzani wajipange,” alisema Inonga.

SOMA NA HII  KUPITIA EXPANSE STUDIO...MERIDIANBET WANAKUJIA NA SLOT YA KIJANJA YA ROULETTE...