Home Azam FC KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI….AZAM FC WAAMUA KUIFANYIA ‘MAJAMBOZI’ YA UHAKIKA YANGA...

KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI….AZAM FC WAAMUA KUIFANYIA ‘MAJAMBOZI’ YA UHAKIKA YANGA SC…


Azam FC imeichungulia Yanga na kuangalia rekodi yao kwa mechi mbili zilizopita za msimu uliopita na fasta benchi la ufundi la timu hiyo kuanza kujipanga mapema, ikitaka mechi za kirafiki kabla ya kuvaana na watetezi hao katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Septemba 6.

Makocha wa timu hiyo inayoshika nafasi ya tano kwa sasa ikiwa na pointi nne kupitia mechi mbili za awali za ligi hiyo, wamesema wanataka kutumia mapumziko ya wiki mbili wakati ligi imesimama ili kujiweka fiti.

Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema Azam itakuwa Amaan, Zanzibar kuvaana na Taifa Jang’ombe iliyowaalika katika tamasha lao na Jumanne ijayo itakwaruzana na As Arta Solar 7 ya Djibouti katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayopigwa Azam Complex, jijini Dar.

Kocha wa timu hiyo, Abdihamid Moallin alisema mechi hizo za kirafiki zitamsaidia kuboresha kikosi chake kabla ya kukutana na Yanga na ni muhimu kushinda.

SOMA NA HII  BAADA YA OKRAH...ANAYEFUATIA KUTAMBULISHWA YANGA NI HUYU HAPA...JAMAA ANAJUA MNOO..