Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWA NAHODHA…MAGUIRE MAMBO YAWA MAGUMU MAN UTD…KOCHA WAKE ATOA KAULI...

PAMOJA NA KUWA NAHODHA…MAGUIRE MAMBO YAWA MAGUMU MAN UTD…KOCHA WAKE ATOA KAULI NZITO ….


Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag ametoa kauli nzito kuhusu hatima ya nahodha wa klabu hiyo muingereza Harry Maguire.

Ten Hag amesema licha ya kuwa Maguire ni Nahodha wake lakini hiyo pekee haimpi uhakika wa kuanza kila mchezo.

“Nalisema hili haimanishi unapokuwa Nahodha basi unakuwa na haki ya kucheza kila mchezo hasa pale unapokuwa na Varane katika kikosi chako.” amesema Ten Hag akimuongelea Maguire.

Aidha katika hatua nyingine Kocha huyo raia wa Uholanzi amemmwagia sifa beki wa zamani wa real Madrid ambaye kwa sasa yupo katika kikosi chake cha Manchester United Rafael Varane kwa kubainisha kuwa hadhi aliyonayo na mafanikio aliyoyapata yana mchango mkubwa sana ndani ya kikosi hicho.

“Hadhi yake, mafanikio yake na yote aliyoshinda inaonesha kuwa anaweza kuwa na mchango mkubwa sana ndani ya kikosi chetu. Kwa upande wa timu kuna ushindani mkubwa na kuna michezo mingi na tunaweza kuona kila baada ya mchezo kujua ni nini hasa tunahitaji.”

Manchester United imekusanya jumla ya alama tatu katika michezo yake mitatu ya mwanzo ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufunga klabu ya Liverpool kwa jumla ya mabao 2-1, huku ikiwa imetoka kupoteza michezo yake miwili dhidi ya Brighton and Hove Albion pamoja na Brentford.

SOMA NA HII  ULIIKOSA BILIONI MOJA YA SportPesa YA JACKPOTI ILIYOPITA..?..SASA MZIGO UMERUIDISHWA TENA...CHEZA KWA BUKU TU...