Home Uncategorized KAHATA: NINAAMINI TUTAPITA SALAMA KATIKA HILI

KAHATA: NINAAMINI TUTAPITA SALAMA KATIKA HILI

FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa imani yake ni kwamba siku moja kila kitu kitakuwa sawa kwa msaada wa Mungu.

Kahata yupo nchini Kenya ambapo alikwenda kwa ajili ya mapumziko baada ya ligi ya Bongo kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Bado kuna matumaini siku moja kila kitu kitakuwa sawa na maisha yataendelea kama kawaida kikubwa ni kuchukua tahadhari na Mungu atatusaidia tutapita salama,” .

Kahata ni ingizo jipya ndani ya Simba ambapo alisajiliwa akitokea Klabu ya Gor Mahia ambao wamepewa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya baada ya ligi yao kufutwa kutokana na janga la Corona.

SOMA NA HII  COASTAL UNION YAAMBULIA POINTI TATU KWA MARA YA KWANZA VPL