Home Uncategorized LIPULI YAFICHUA KILICHOWAPONZA MBELE YA AZAM FC

LIPULI YAFICHUA KILICHOWAPONZA MBELE YA AZAM FC


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa kilichowaponza wakapoteza mchezo wao wa fainali mbele ya Azam FC jana uwanja wa Ilulu ni kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.


Lipuli ilikubali kupoteza dakika ya 64 baada ya mlinda mlango wa Azam FC, Razack Abarola kupiga pasi ndefu iliyomkuta Obrey Chirwa aliyemshinda beki wa Lipuli Haruna Shamte, kabla ya kuachia shuti kali lililozama wavuni.

Matola amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na mipango yao ilikuwa kutwaa ubigwa walizidiwa mbinu na wapinzani wao.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu, tumepambana kwa kutafuta matokeo mwisho wa siku tumepoteza. haikuwa mipango yetu kufikia hapa ila ni matokeo na kwenye fainali lazima bingwa apatikane,” amesema Matola.
SOMA NA HII  KOCHA YANGA: NTIBAZONKIZA HANA KAZI YA KUFUNGA