Home Uncategorized KINDOKI WA YANGA KUIBUKIA TIMU HII TPL

KINDOKI WA YANGA KUIBUKIA TIMU HII TPL

IMEELEZWA kuwa mlinda mlango namba moja wa kikosi cha Yanga, Klaus Kindoki anawindwa na klabu ya Singida United ili kuongeza nguvu upande wa ulinzi msimu ujao.

Kindoki raia wa Congo hajawa na msimu mzuri kwenye kikosi hicho kutokana na kufanya makosa mengi ya kiufundi hali iliyosababisha kuwe na taarifa kwamba huenda msimu huu klabu hiyo ikaachana na mlinda mlango huyo na imeelezwa tayari Singida United wamepeleka maombi kumpata mchezaji huyo.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa bado kwa sasa mipango haijawa wazi hasa kwa upande wa usajili kutokana na kusubiri ripoti ya mwalimu.

“Suala la usajili kwa timu yetu kwa sasa michakato haijaanza, ripoti ya mwalimu ikipita tutafanyia kazi mapendekezo yake hivyo kwa sasa mambo bado,” amesema Katemana.

Endapo dili la Kindoki litakamilika basi mlinda mlango huyo atabaki kwenye ligi msimu huu akiwa na kikosi cha Singida United ambacho kilikuwa kwenye hatihati ya kushuka daraja msimu uliopita.

SOMA NA HII  KIPA NAMUNGO FC AINGIA ANGA ZA MTIBWA SUGAR NA RUVU