Home Habari za michezo CHAMA AWEKA REKODI YA KIBABE NYUMBANI

CHAMA AWEKA REKODI YA KIBABE NYUMBANI

Habari za Simba

Clatous Chota Chama ama Mwamba wa Lusaka kama wengi wanavyopenda kumwita, alikuwa katika ardhi ya Nyumbani kwao Zambia, katika jiji la Ndola.

Chama mzaliwa wa mji wa Mansa, Makao Makuu ya jimbo la Luapula, jana alikuwa na jukumu la kuhakikisha Simba SC, haiondoki kichwa chini ndani ya ardhi ya nchi yake.

Wakati Mnyama akiwa nyuma kwa goli moja, Chama akaukwamisha wavuni mpira dakika 59 na kuweka mizania sawa.

Dakika 74 Simba ikawa nyuma tena na ubao ukisomeka 2-1, Clatous akatumia mguu wake wa kushoto na kuiandikia bao la kusawazisha dakika ya 90 kufanya mambo kuwa 2-2.

Ukikutana na Mwamba huyu leo, neno gani ungetamani kumwambia?

SOMA NA HII  UCHOCHORO WA SIMBA KUWA KIBONDE UKO HAPA