Home Habari za michezo KISA SARE NA POWER DYNAMO JANA….MBRAZILI SIMBA APATA CHA KUJITETEA….

KISA SARE NA POWER DYNAMO JANA….MBRAZILI SIMBA APATA CHA KUJITETEA….

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba , Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema wamepoteza nafasi tano za wazi za kufunga katika sare ya 2-2 dhidi ya Power Dynamos ambazo zingetuwezesha kupata ushindi mnono ugenini.

Robertinho amesema kipindi cha pili timu yake ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi ambazo hwakuzitumia vizuri.

Hata hivyo Robertinho amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya katika mchezo wa jana licha ya kupata sare.

“Tumecheza vizuri hasa kipindi cha pili, tumetengeneza nafasi nyingi. Tumepoteza nafasi zaidi ya tano za kufunga lakini huu ndio mpira wa miguu tunarudi nyumbani kujipanga,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake, mlinzi wa kati Che Fondoh Malone amesema bado wanafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam hivyo wanarudi kujipanga.

“Hatujakata tamaa ya kusonga hatua ya makundi, tuna dakika 90 nyingine nyumbani ambazo tunaamini tutazitumia vizuri na kuingia hatua ya makundi,” amesema Che Malone.

SOMA NA HII  BOCCO ATAMBA NYUMBANI MATOKEO MAZURI UHAKIKA