Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA CHIRWA…IHEFU FC WAMTAGETI YONDANI …JUMA NYOSO ZAMAANI ‘KASHASINYA’...

BAADA YA KUMALIZANA NA CHIRWA…IHEFU FC WAMTAGETI YONDANI …JUMA NYOSO ZAMAANI ‘KASHASINYA’ KATABA NONO…


BAADA ya mabosi wa Ihefu FC kumalizana na Obrey Chirwa inaelezwa kuwa anayefuata ni beki kitasa Kelvin Yondani ambaye ni mali ya Geita Gold.

Ihefu ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara inajiimarisha kwa ajili ya msimu mpya ikiwa ni mpango wa kufanya kweli ndani ya ligi kuepuka kushuka daraja kama ilivyokuwa msimu wa 2019/20 na kushiriki Championship.

Habari zimeeleza kuwa Ihefu wamefikia hatua nzuri na Yondan hivyo kilichobaki ni kuweza kumtambulisha ikiwa makubaliano yatakuwa sawa.

“Ihefu hawana jambo dogo wanataka kufanya kweli,tayari wamemalizana na baadhi ya wachezaji wenye uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na Yondani,kilichobaki ni kumalizia makubaliano ya mwisho na kuwatambulisha,” ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Ihefu FC,Peter Andrew amesema kuwa usajili bado unaendelea kwa ajili ya kuimarisha kikosi.

“Bado tunaendelea kuimarisha kikosi na kusajili hivyo kazi ikikamilika tutawatangaza na ikumbukwe kwamba tayari wachezaji wameanza mazoezi.

“Chirwa tayari ameshatangazwa rasmi na ni mchezaji wetu kuhusu Yondan hiyo taarifa bado hatuna,” amesema.

Chirwa na Yondani waliwahi kucheza wote ndani ya kikosi cha Yanga wataungana na Peter Mwalyanzi ambaye ni mshambuliaji pamoja na kiungo Jaffary Kibaya na beki Juma Nyosso ambao tayari wameshatambulishwa.

SOMA NA HII  STAA HUYU WA SIMBA ANAJUTA KUONDOKA YANGA, STORI KAMILI IKO HIVI