Home Habari za michezo HUKO SUPER LEAGUE MAMBO NI MOTO, SIMBA WAJA NA MBINU HII KUIMALIZA...

HUKO SUPER LEAGUE MAMBO NI MOTO, SIMBA WAJA NA MBINU HII KUIMALIZA AL AHLY

Habari za Simba

Simba watavaana na Al Ahly ya Misri katika michuano ya African Super League hatua ya nane bora.

Bila shaka Simba wanafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa wanafanya vyema katika michuano hiyo Mikubwa Afrika.

Licha ya hivyo kuna vitu ambavyo Simba inabidi wajiweke sawa ili kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo huo.

Simba wanahitaji kufanyia kazi sana vitu kadhaa na basi watakuwa wamejipa nafasi kwenye mikondo miwili dhidi ya Ahly, Nyumbani watatakiwa waende wakiwa tayari na Tempo yao ya juu, muunganiko imara, kuonana kwa haraka na kwa pasi sahihi kwenye mchezo na umakini kwa dakika 90 kwa walinzi na golikipa.

Wakiwa ugenini watahitaji kuwa na ustadi kwenye kuzuia (Defensive prowess), matumizi ya nafasi bila hiyana na bahati pia.

Miquissone ni mchezaji wa mechi muhimu, Simba wakimpata Miquissone alie timamu na atakaeamka kwenye mood ya mechi muhimu basi wanazidi kujiongezea nafasi hasa kwa Mkapa.

SOMA NA HII  SAMATTA AWATAMBIA WA NIGER KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA