Home Habari za michezo MANULA ATAKA NAFASI YAKE SIMBA, ISHU IKO HIVI

MANULA ATAKA NAFASI YAKE SIMBA, ISHU IKO HIVI

Aishi Manula anaitaka nafasi yake! Anataka kutuonesha ukubwa wa daraja lake akiwa anaheshimu ubora wa waliopo.

Mtaalamu wa Sayansi ya michezo Mikael Igendia faida yake imeonekana. Wachezaji walikuwa wakikaa nje muda mrefu mpaka mikataba inavunjwa au mpaka muda uliotangazwa ufike na bado wakirudi wanahitaji tena muda.

Lakini Aishi ameweza kukanyaga nyasi tangu mwezi uliopita akiwa anakisiwa kurudi October.

Tayari anaendelea kujifua peke yake na kurudi kwake anakutana na ushindani wa magolikipa watatu Ayoub Lakred, Ally Salim ambae anafanya vyema hivi sasa na Ismail Abel aliesajiliwa kutokea KMC.

Je Manula atafanikiwa kurudi katika lango la Simba SC?

SOMA NA HII  GOMES: TUNA SAFU BORA YA ULINZI