Home Uncategorized AUBAMENYANG ACHEKELEA KUWATUNGUA EVERTON, SASA AFIKISHA MABAO 17

AUBAMENYANG ACHEKELEA KUWATUNGUA EVERTON, SASA AFIKISHA MABAO 17


Pierre-Emerick Aubameyang, nahodha wa timu ya Arsenal amesema kuwa ni furaha kwa timu yake kushinda mchezo wao mbele ya wapinzani Everton.

Aubameyang alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-2 walioupata jana wakiwa nyumbani, Emirates.

Nahodha huyo amesema:”Ni furaha kwetu kushinda hakuna kingine tunachokifikiria zaidi ya kuona timu inashinda kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,”.

Mabao hayo mawili yanamfanya nyota huyo kufikisha jumla ya mabao 17 kwenye Ligi Kuu England.

SOMA NA HII  MORRISON ATAJWA KUWA TISHIO ZAIDI YANGA, KOCHA AANIKA SABABU