Home Uncategorized RATIBA YA KUKUSANYA KIJIJI YA YANGA IPO NAMNA HII

RATIBA YA KUKUSANYA KIJIJI YA YANGA IPO NAMNA HII

TIMU ya Yanga kuelekea siku ya Mwananchi ambayo inatarajiwa kuwa Agosti 4 uwanja wa Taifa ambapo watacheza na mabingwa wa SportPesa Cup Kariobarg Sharks ratiba yao ipo namna hii:-

Julai 29 Msafara ulipokelewa na wanachama wa Bagamoyo eneo la Mapinga kwa maandamano majira ya saa tatu asubuhi

Julai 30 msafara utakuwa Viwanja vya Sabasaba (Kiwanja cha Ndege) Morogoro Mjini. Mapokezi yatakuwa saa tatu asubuhi kupitia njia ya Old Dar es Salaam Road hadi njia panda ya Bigwa kuelekea Kilakala na kuingia njia ya Kichangani hadi Mji Mpya kuelekea Nunge kupitia daraja la Mwere hadi round about ya Posta na Round about ya Stand ya daladala. 


Msafara utaelekea Msamvu kuelekea Chamwino hadi Mafiga na kutokea Sua Road hadi round about ya Sua na kumalizia kukusanya Kijiji katika katika Kiwanja cha ndege – Sabasaba.

Julai 31
Msafara utakuwa Chalinze Mjini Nyuma ya Polisi.
Mapokezi yataanzia Mdaula saa tatu asubuhi kwa msafara hadi Chalinze viwanja vilivyopo nyuma ya Kituo cha Polisi Chalinze.

Agosti Mosi
Mlandizi mjini 


Msafara utapokelewa Ruvu Darajani hadi viwanja vya wazi Mlandizi.

Agosti 02
Kibaha Maili Moja
Msafara utapokelewa kwa Kibaha kwa Mathias kupitia Picha ya Ndege hadi Stand ya Mabasi Kibaha Maili moja (Kibaha Container)

Agosti 3


Kigamboni Uwanja wa Swala Tuamoyo.

Msafara utapokelewa Darajani Kurasini kuelekea Viwanja vya Swala Tuamoyo. 


Pia utaratibu wa kuipokea timu kutoka Morogoro utapokelewa na watu wa mkoa wa Pwani kabla ya timu kukabindhiwa kwa wana Dar utakuwa chini ya Katibu wa Hamasa wa Yanga, Deo Muta.

SOMA NA HII  VIGONGO VINNE VYA MOTO KWA YANGA HIVI HAPA