Home Habari za michezo AHMED ALLY:- WACHEZAJI WETU NDIO CHANZO CHA YOTE HAYA…

AHMED ALLY:- WACHEZAJI WETU NDIO CHANZO CHA YOTE HAYA…

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klanbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kejeli ambazo mashabiki wa timu hiyo wanazipata hivi sasa zimesababishwa na wachezaji wao baada ya kufungwa na watani zao bao 5-1 kisha mchezo uliofuata wakatoa sare na Namungo FC kwa bao 1-1.

Ahmed amesema hayo leo Novemba 16, 2023 wakati akizindua kampenzi ya hamasa kuelekea mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023 katika Dimba la Mkapa.

“Wachezaji lazima watambue kwamba kejeli zote ambazo Simba tunazipata mtaani hivi sasa zimesababishwa na wao. Kwa hiyo wao wanayo kazi kubwa ya kutufutia hizi kejeli kwa kufanya vizuri katika mchezo ujao.

“Tukipata matokeo mazuri kwenye mchezo huo itapunguza machungu makubwa ambayo wanasimba wanapitia hivi sasa na kupunguza sehemu kubwa ya kejeli tunazozipata. Hii kadhia tunayoipata wameisababisha wao, na wanayo kazi ya kufanya kuiondoa hii shida, hatuna mashaka na ubora wao.

“Waone ni kwa namna gani mashabiki wa Simba wanaumia na kuteseka na wao ndio wafariji wakuu. Niwaambie wachezaji watakapokuwa wanakuja Uwanjani Novemba 25, wakifika uwanjani kabla ya kuingia ndani wafungue vioo vya gari waone mstari wa foleni ya mashabiki ulivyo mrefu.

“Mtu amekaa tangu asubuhi mpaka saa 8 hajaingia uwanjani, sababu anakuja kuiona Simba yake. Tuwaonee huruma wote wanaojitoa kuipambania Simba, wanaotoka mikoani kuja kuishuhudia Simba, waende wajapambane kweli Simba irejeshe heshima yao,” amesema Ahmed Ally..

SOMA NA HII  ISHU YA UWEKEZAJI SIMBA YAJA KIVINGINE, SERIKALI YATOA TAMKO