Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU…HIVI NDIVYO MABOSI WA YANGA WALIVYOTUA ALGERIA KININJA..

KUELEKEA MECHI NA WAARABU…HIVI NDIVYO MABOSI WA YANGA WALIVYOTUA ALGERIA KININJA..

Habari za Yanga

Mabosi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans mwanzoni mwa juma hili waliondoka jijini Dar es salaam kuelekea nchini Algeria, kwa ajili ya kuwaangalia wapinzani wao CR Belouizdad wakiongozana na mchamnbuzi wa video, Khalil Ben Youssef.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Novemba 24, mwaka huu katika mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, utakaopigwa nchini Algeria.

Young Africans imepania kufanya vema katika michuano hiyo ya kimataifa msimu huu, baada ya ule uliopita kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Algiers.

Mmoja wa mabosi kutoka Kamati ya Mashindano ya Young Africans amesema, wamesafiri kwenda Algeria kwa ajili ya kuwaangalia CR Belouizdad ambao watacheza michezo miwili ya ligi kabla ya kukutana na Young Africans.

Bosi huyo amesema chini ya mchambuzi huyo wa video, wataitumia michezo hiyo kuwaangalia wapinzani wao kwa lengo la kuona ubora na udhaifu walionao Belouizdad.

Ameongeza kuwa, anaamini mchambuzi huyo ataisoma vema kiufundi na kimfumo na baadae kukabidhi ripoti kwa Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake.

“Mchambuzi wetu wa video ndani ya timu, Youssef pamoja na baadhi ya viongozi tayari wamewasili nchini Algeria ili kuwasoma wapinzani wetu CR Belouizdad.

“Youssef akiwa huko ataisoma CR Belouizdad kiufundi zaidi kwa kimfumo na kimuundo na ripoti itarudi mapema kwa Gamondi kwa ajili ya kuipitia.

“Gamondi ataitumia ripoti hiyo kumuongoza katika kukiandaa kikosi chake, kabla ya kukutana na CR Belouizdad,” amesema bosi huyo.

Rais wa Young Africans, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alizungumzia mipango ya timu hiyo, msimu huu katika michuano ya kimataifa na kusema kuwa: “Malengo yetu ni makubwa msimu huu katika michuano ya kimataifa, msimu uliopita tulicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na huu, tunataka kufika Robo au ikiwezekana tucheze fainali.”

SOMA NA HII  ENDELEA KULA PENSHENI YA USHINDI KUPITIA MKEKA WA MAMILIONI YA MERIDIANBET..