Home Habari za Simba Leo SIMBA HUWAMBIII KITU KWA MONZU…ONANA AITWA KAMBINI

SIMBA HUWAMBIII KITU KWA MONZU…ONANA AITWA KAMBINI

Habari za Simba- Elie Mpanzu

BAADA ya AS Vita kupindua meza dakika za jioni katika dili la winga Mkongomani Elie Mpanzu na Simba, wekundu hao wa Msimbazi wameendelea kumganda staa huyo hadi kieleweke.

Awali Simba na Mpanzu walikubaliana kusaini mkataba wa miaka miwili lakini baadae vigogo wanaommiliki Mpanzu akiwemo moja ya matajiri wapya wa AS Vita, aliingilia kati dili hilo na kumzuia winga huyo kusaini.

Dili la kumsajili winga huyo wa AS Vita lina ugumu kutoka kwenye timu, licha ya mchezaji mwenyewe kuonesha nia ya kucheza soka nje ya DR Congo.

Rais wa AS Vita Amdou Diaby aliingilia kati usajili wa nyota huyo kwenda Simba, na kumsihi mchezaji husika kusalia klabuni hapo na atampa mara tatu ya kile kinachotolewa na Simba. Inaelezwa kwamba Uongozi wa AS Vita wameiambia Simba itoe Dola 150000 zaidi ya Tsh Milioni 600 ili kumsajili mchezaji huyo.

Lakini Elie Mpanzu mwenyewe inaeleza kishawaaga wachezaji wenzake, na kinachosubiriwa tu ni makubaliano kati yake na Uongozi wa timu yake.

Inaelezwa kwamba Kiongozi mmoja wa Simba alifika DR Congo kusukuma dili hilo, na kumchukua mchezaji huyo kumpelea Kinshasha kuepuka hatari ya mashabiki ambao nao hawataki aondoke.

Uongozi wa Simba imelazimika sasa kumtafuta Willy Onana ambay ametakiwa kuripoti kambin haraka, awali Simba walitaka kumuacha lakini muda huu Onana yupo Da tayari kwa kuanza safari ya kujiunga na wenzake MISRI.

Simba hadi sasa imefanya sajili 11, huku ikianza na Joshua Mutale, Steve Mukwala, Jean Charles Ahoua, Augustine Okejepha, Abdulrazak Hamza, Valentino Mashaka, Deborah Farnandes, Valentine Nouma, Yusuph Kagoma, Chamou Karaboue, Lameck Lawi.

Na bado inaelezwa wataendelea kutambulisha vyuma vya kaz, ikiwa leo watatambulisha Mashine ya Ubaya Ubwela kwa mujibu wa Afisa Habari wa Klabu hiyo Ahmed Ally.

SOMA NA HII  YUSUF MANJI TAJIRI WA YANGA KUZIKWA LEO...YANGA KUMUENZI KWA MAMBO 9.