Home Uncategorized DAN ALVES ATANGAZA KUACHANA NA PSG

DAN ALVES ATANGAZA KUACHANA NA PSG


Mlinzi wa kulia wa klabu ya Paris Saint-Germain, Dani Alves ametangaza kuihama klabu hiyo majira haya ya joto

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Alves mwenye umri wa miaka 36 amesema kuwa anaweza kuanza maisha mapya msimu wa 2019/20 ingawa hajaweka wazi ni klabu gani ataenda.

“Ukurasa mwingine mpya kwenye maisha yangu unafungwa leo, ukurasa wenye mafanikio ambao nimejifunza na kuongeza uzoefu.

“Ningependa kuishukuru familia nzima ya PSG kwa fursa tuliyoipata pamoja ya kuweka historia mpya kwenye klabu hii,” ilisema taarifa hiyo.

Alves ameyasema hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Brazil na Peru ambao alikuwa nahodha huku akifanikiwa kufunga moja ya mabao kwenye ushindi wa mabao 5-0 na kuiongoza timu yake kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America.

Alves alijiunga na PSG majira ya joto mwaka 2017 akitokea klabu ya Juventus ambayo alidumu kwa mwaka mmoja tu

Mbali na Juventus, Alves pia ameshacheza kwenye vilabu vya Sevilla na Barcelona ambapo alitwaa mataji kadha wa kadha.

Taarifa zinadai kuwa huenda nyota huyo akasajiliwa na moja ya vilabu vikongwe nchini Uingereza huku wachambuzi wa michezo wakiwa na shaka iwapo kama mbrazili huyo ataweza kuendana na kasi na kiwango cha nguvu ambacho hutumika kwenye Ligi hiyo kutokana na umri wake.

SOMA NA HII  KUBETI KWAMPONZA STURRIDGE, FA, FA ZAMFUNGIA, KLABU YAKE YAMTEMA