Home Uncategorized SARPONG ACHEKELEA KUIBUKIA YANGA, ATOA AHADI HII

SARPONG ACHEKELEA KUIBUKIA YANGA, ATOA AHADI HII

Habari za Yanga


MICHAEL Sarpong mchezaji mpya wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anafurahi kujiunga na Yanga na anaamini kwamba atapambana kufikia malengo ya timu hiyo.

Sarpong raia wa Ghana yeye ni mshambuliaji amemalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili na anatarajiwa kutambulishwa rasmi Agosti 30 kwenye kilele cha Wiki ya Wananchi Uwanja wa Mkapa.


Anaungana na wachezaji wengine wawili ambao ni Tusila Kisinda na Tunombe Mukoko ambao wanatarajiwa kuanza rasmi mazoezi kesho, kuungana na wachezaji wenzao ambao tayari walishaanza mazoezi tangu Agosti 10.


Nyota huyo amesema:”Ninafurahi kuwa mwanafamilia wa Yanga ninatambua kwamba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wazuri hivyo nitakachofanya ni kutimiza majukumu yangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu.” 

SOMA NA HII  NYOTA SABA MATATA WAMPASUA KICHWA MBELGIJI WA SIMBA