Home Habari za michezo KUMBE SIMBA NA ZORAN WALIKUWA WANAVIZIANA BANA…HIZI HAPA SABABU 7 ZILIZOPELEKEA BARBARA...

KUMBE SIMBA NA ZORAN WALIKUWA WANAVIZIANA BANA…HIZI HAPA SABABU 7 ZILIZOPELEKEA BARBARA KUKUBALI AONDOKE…


Simba imeachana na Kocha Mserbia, Zoran Maki siku 70 baada ya kumsaini mkataba wa mwaka mmoja Juni 28 kwa makubaliano ya kutetea vikombe vyote na kufika nusufainali ya Klabu Bingwa Afrika. Sambamba na huyo pia imewatema Kocha wa viungo, Sbai Karim na yule wa makipa Mohammed Rachid ambao wote walikuwa wasaidizi wake na alikuja nao.

Habari za uhakika ni kwamba kuna sababu 7 zilizomng’oa Kocha huyo ndani ya Simba ambayo aliisimamia kwenye mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold(3-0) na Kagera Sugar(2-0) na anaongoza ligi.

Lakini taarifa ya klabu iliyotolewa adhuhuri, ilisema kwamba pande zote mbili zimekubaliana kusitisha mkataba na Kocha Mzawa, Seleman Matola ndiye atakayeiongoza timu hiyo dhidi ya KMC leo usiku kwenye Uwanja wa Mkapa.

Hata hivyo habari za ndani ya Simba zinasema Matola ambaye ni mchezaji wa zamani wa Wekundu hao alikuwa hapewi ushirikiano mkubwa na Zoran ambaye alikuwa kama anashinikiza aongezewe nguvu ya wasaidizi wake zaidi ya aliowakuta kwenye benchi. Habari zinasema kwamba tayari Simba imeshaanza mchakato wa Kocha mpya na ndani ya wiki mbili atakuwa Dar es Salaam.

SABABU ZENYEWE

1-OFA YA AL ITTIHAD

Habari za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu wa Zoran ni kwamba tangu wikiendi alishamalizana na Ittihad ya Misri na jana asubuhi alikutana na viongozi wa Simba na kuwaeleza kutoridhishwa na baadhi ya mambo na kuomba kusitisha mkataba yeye na wasaidizi wake. Hata hivyo saa nne baada kumalizana na Simba alitangazwa kuwa kocha wa timu hiyo.

2-ONYANGO NA BOCCO

Presha za kutocheza kwa wachezaji John Bocco na Joash Onyango ilikuwa mzigo mzito kwa kocha huyo kwa madai kwamba kila mara viongozi waandamizi walikuwa wakishinikiza hilo. Onyango aliondoka kambini huku Bocco akisalia lakini hakutumika.

3-NGUVU YA MASTAA

Baadhi ya mastaa inaelezwa kwamba walimkera kocha huyo kwavile walikuwa wakikimbilia zaidi kudeka kwa viongozi na walisikilizwa huku Kocha huyo akitaka mambo yote yaishie kwake.

SOMA NA HII  KANOUTE ATAMBA AFL AWEKA REKODI HII MPAKA SASA

4-MECHI ZA KIRAFIKI

Habari za ndani zinadai kwamba Zoran aliwakera viongozi baada ya kutaka kuweka ngumu timu isiende Sudan kwenye mechi za kirafiki lakini hata iliporudi Dar akataka kugomea mechi ya Solar Arta 9 ya Djibout ambayo Simba ilipoteza.

5-MALAZI

Habari zinadai kwamba kumekuwa na mzozo wa chinichini katika siku za hivikaribuni baina ya uongozi, kocha huyo na wasaidizi wake kuhusiana na makazi yao ambapo walikuwa wakishinikiza kutafutiwa nyumba za kifahari.

6-MASILAHI

Habari zinasema kwamba Zoran alikuwa akidai baadhi ya vitu ambavyo alikuwa hajakamilishiwa kwenye mkataba wake, ingawa inadaiwa kwamba muda ulikuwa bado.

7-MZOZO NA WAANDAMIZI

Inasemekana kwamba Zoran amekuwa na mizozo na mara kadhaa na baadhi ya viongozi kuhusiana na mambo ambayo hawaridhiki nayo lakini amekuwa haambiliki.

Lakini hata misimamo yake kuhusiana na upangaji wa vikosi kumkomalia beki Outara umemponza kwani amekuwa hampi kiwango bora.