Home Habari za michezo WAKATI WAKIJINDAA NA SINGIDA BIG STARS….MASUDI DJUMA KAJIPIGA PIGA KIFUANI ..KISHA KWA...

WAKATI WAKIJINDAA NA SINGIDA BIG STARS….MASUDI DJUMA KAJIPIGA PIGA KIFUANI ..KISHA KWA JEURI AKASEMA HAYA…


Kocha Masoud Djuma Irambona amesema yupo tayari kwa mchezo wa Mzunguuko watatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars.

Kocha huyo kutoka Burundi amesema amekitumia vizuri kipindi cha majuma mawili ambacho Ligi Kuu ilisimama, kurekebisha baadhi ya makosa ambayo yalipelekea kupoteza michezo miwili ya awali msimu huu.

Amesema anatambua mchezo dhidi ya Singida Big Stars utakua na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa kikosi cha wapinzani wao, lakini kwake anaamini umefika wakati kwa wachezaji wake kuthibitisha ubora wao.

“Dodoma Jiji ni klabu kubwa, tuna wachezaji wazuri ninaamini watatumia maarifa na kufuata nilichowafundisha wakati ligi imesimama, nimebaini baadhi ya mambo ambayo yalitukwamisha kwenye michezo iliyopita.”

“Huenda ikawa sijatatua matatizo yote lakini asilimia kubwa nina uhakika kuna mabadiliko ambayo yataanza kuonekana katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Singida Big Stars.” amesema Kocha Masoud ambaye aliwahi kupita Simba SC kama Kocha msaidizi.

Singida Big Stars itakua nyumbani Uwanja wa Liti mjini Singida kucheza dhidi ya Dodoma Jiji FC keshokutwa Jumamosi (Sepetamba 11).

SOMA NA HII  WEEKEND INAKUJA NA MAOKOTO NAYO YANAZIDI KUONGEZEKA...WEKA MKEKA WAKO HAPA..