Home Habari za michezo HAYA SASA NI SIMBA HAPO SEPTEMBER 14

HAYA SASA NI SIMBA HAPO SEPTEMBER 14

Habari za Simba

Wawakilishi wa Tanzania Bara Kimataifa Simba SC wanatarajia kuondoka nchini Septemba 14, mwaka huu kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Power Dynamos.

Power Dynamos itawakaribisha Simba SC katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Mzunguuko wa Pili wa michuano hiyo utakaochezwa Septemba 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa ulioko katika mji wa Ndola.

Akizungumza jijini Dar es salaam Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally, amesema kikosi cha timu hiyo kinaendelea vyema na mazoezi na wachezaji wataingia kambini rasmi leo Jumamosi (Septemba 09) ili kuongeza umakini.

Ahmed amesema wanataka kuona kila mchezaji anakuwa imara na tayari kwa ajili ya mechi hiyo wetu muhimu.

Amesema wachezaji wote wako vizuri na tayari Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, ametoa majukumu ‘mazito’ kwa wachezaji wake baadhi akiwamo winga machachari, Aubin Kramo.

“Wachezaji wote wapo sawa na wanaendelea vizuri na programu zangu isipokuwa kwa wale ambao wapo katika majukumu ya timu zao za taifa, tumepata muda mrefu wa kukamilisha mambo ya msingi kuelekea katika mchezo wetu wa Zambia, kitu kizuri tunaenda kucheza na mpinzani tunayemfahamu vyema, hatuhitaji kupuuzia kwa sababu tunawafahamu.

Matarajio yetu ni kuongeza nguvu kubwa katika mazoezi kutokana na majukumu ambayo kila mchezaji tumempatia ili kufikia malengo,” amesema Ahmed.

Simba SC iliwaalika Power Dynamos katika Tamasha la Simba Day na katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa wenyeji walipata ushindi wa mabao 2-0.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AIBUKIA YANGA AMPA GAMONDI MBINU ZA KUIUA AL AHLY