Home Habari za michezo ROBERTINHO AIBUKIA YANGA AMPA GAMONDI MBINU ZA KUIUA AL AHLY

ROBERTINHO AIBUKIA YANGA AMPA GAMONDI MBINU ZA KUIUA AL AHLY

Habari za Michezo

Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa pili wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, huku kocha wa zamani wa Simba aliyewabana Wamisri hao kwenye mechi mbili za Football League (AFL), Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameipa ujanja ili kuweza kuibana Kwa Mkapa.

Robertinho, aliilazimisha Al Ahly sare ya mabao 2-2 katika mechi ya kwanza nyumbani kisha kwenda kutoka nao sare ya 1-1 jijini Cairo na kutolewa hatua ya robo fainali kwa faida ya mabao ya ugenini kabla ya kufurushwa na mabosi wa Msimbazi baada ya kipigo cha mabao 5-1 ilichopewa na Yanga, Novemba 6.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu akiwa njiani kwenda Saudi Arabia kwa mapumziko Robertinho alisema Yanga kama inataka kushinda mechi hiyo lazima ijipange kwa kutumia mifumo miwili kwa wakati mmoja.

Robertinho alisema Yanga inaweza kuimaliza Al Ahly kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1 wakati wakiwa hawana mpira lakini watakapokuwa wanashambulia wanaweza kubadilika na kutumia 4-3-3 ili kurahisisha mashambulizi.

Pia aliwaongezea madini kuwa, Ahly nao hubadilika wanapokuwa hawana mpira wakitumia mfumo wa 4-2-3-1 lakini wakiwa wanashambulia hutumia ule wa 4-4-2.

“Al Ahly wanacheza tofauti wanapokuwa nyumbani na ugenini kwa kuwa Yanga itaanzia nyumbani, ndio wanatakiwa kuicheza hii mechi kwa kuhitaji matokeo mazuri lakini wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa wapinzani wao wanapenda sana kucheza soka la kushambulia,” alisema Robertinho.

“Kama Yanga watatumia mfumo wa 4-3-3 wakati wa kushambulia utawafanya kuwa na idadi nzuri kule mbele katika mashambulizi yao ambayo itawapa wakati mgumu mabeki wa Al Ahly ambao hawana utulivu sana.

“Ahly hawana kasi sana ya kukimbia kurudi nyuma kujilinda hili lazima Yanga ilitumia kwa kucheza mpira wa kasi ili wafike langoni kwao kuwapa presha mabeki wao.

Pia, Robertinho alisema Yanga ina wachezaji watatu wenye ubora, Stephanie Aziz KI, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli kama wakiamka vizuri siku ya mchezo wanaweza kuwa hatari mbele ya Ahly wakati timu yao ina mpira kutokana na ubora wao wa kujua kukimbia haraka.

“Yanga ina watu wanaojua kukimbia na mpira Aziz KI, yule aliyetunfunga mabao mawili (Maxi) na yule mwenye nywele nyeupe (Pacome) ni wachezaji wazuri wenye kasi kulekekea lango la mpizani kama watakuwa vizuri siku yab mchezo wanatakiwa kuipa wakati mgumu Ahly,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Kama wakiona mechi inakuwa ngumu wasisite kubadilika na kutumia washambuliaji wawili kule mbele ili kuzidi kuwapa presha mabeki wa Ahly ni wazuri lakini wanapitika.”

Yanga itavaana na Al Ahly ikiwa wiki moja tangu inyukwe mabao 3-0 na CR Belouizdad ya Algeria katika mechi ya Kundi D, huku wageni wao wakitoka kushinda idadi kama hiyo dhidi ya Medeama ya Ghana.

KIKOSI cha Yanga kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa pili wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, huku kocha wa zamani wa Simba aliyewabana Wamisri hao kwenye mechi mbili za Football League (AFL), Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameipa ujanja ili kuweza kuibana Kwa Mkapa.

Robertinho, aliilazimisha Al Ahly sare ya mabao 2-2 katika mechi ya kwanza nyumbani kisha kwenda kutoka nao sare ya 1-1 jijini Cairo na kutolewa hatua ya robo fainali kwa faida ya mabao ya ugenini kabla ya kufurushwa na mabosi wa Msimbazi baada ya kipigo cha mabao 5-1 ilichopewa na Yanga, Novemba 6.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu akiwa njiani kwenda Saudi Arabia kwa mapumziko Robertinho alisema Yanga kama inataka kushinda mechi hiyo lazima ijipange kwa kutumia mifumo miwili kwa wakati mmoja.

Robertinho alisema Yanga inaweza kuimaliza Al Ahly kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1 wakati wakiwa hawana mpira lakini watakapokuwa wanashambulia wanaweza kubadilika na kutumia 4-3-3 ili kurahisisha mashambulizi.

Pia aliwaongezea madini kuwa, Ahly nao hubadilika wanapokuwa hawana mpira wakitumia mfumo wa 4-2-3-1 lakini wakiwa wanashambulia hutumia ule wa 4-4-2.

“Al Ahly wanacheza tofauti wanapokuwa nyumbani na ugenini kwa kuwa Yanga itaanzia nyumbani, ndio wanatakiwa kuicheza hii mechi kwa kuhitaji matokeo mazuri lakini wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa wapinzani wao wanapenda sana kucheza soka la kushambulia,” alisema Robertinho.

“Kama Yanga watatumia mfumo wa 4-3-3 wakati wa kushambulia utawafanya kuwa na idadi nzuri kule mbele katika mashambulizi yao ambayo itawapa wakati mgumu mabeki wa Al Ahly ambao hawana utulivu sana.

“Ahly hawana kasi sana ya kukimbia kurudi nyuma kujilinda hili lazima Yanga ilitumia kwa kucheza mpira wa kasi ili wafike langoni kwao kuwapa presha mabeki wao.

Pia, Robertinho alisema Yanga ina wachezaji watatu wenye ubora, Stephanie Aziz KI, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli kama wakiamka vizuri siku ya mchezo wanaweza kuwa hatari mbele ya Ahly wakati timu yao ina mpira kutokana na ubora wao wa kujua kukimbia haraka.

“Yanga ina watu wanaojua kukimbia na mpira Aziz KI, yule aliyetunfunga mabao mawili (Maxi) na yule mwenye nywele nyeupe (Pacome) ni wachezaji wazuri wenye kasi kulekekea lango la mpizani kama watakuwa vizuri siku yab mchezo wanatakiwa kuipa wakati mgumu Ahly,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Kama wakiona mechi inakuwa ngumu wasisite kubadilika na kutumia washambuliaji wawili kule mbele ili kuzidi kuwapa presha mabeki wa Ahly ni wazuri lakini wanapitika.”

Yanga itavaana na Al Ahly ikiwa wiki moja tangu inyukwe mabao 3-0 na CR Belouizdad ya Algeria katika mechi ya Kundi D, huku wageni wao wakitoka kushinda idadi kama hiyo dhidi ya Medeama ya Ghana.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...MTIBWA SUGAR WASHTUKA JAMBO...WAANZA KUTEMBEA NA 'BITI' LA SIMBA NA YANGA...