Home Uncategorized AJIBU KUTANGAZWA SIMBA LEO

AJIBU KUTANGAZWA SIMBA LEO


Kuna uwezekano mkubwa aliyekuwa mchezaji wa Yanga kwa msimu uliomalizika hivi karibuni, Ibrahim Ajibu akatangazwa kusajiliwa na Simba.

Taarifa zinasema kuwa Ajibu tayari ameshamalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao.

Jana Simba walimtangaza Beno Kakolanya ambaye aliachwa na Yanga kufuatia amdai ya fedha zake za mishahara na zile za usajili.

Endapo Ajibu atatangazwa atakuwa anarejea rasmi katika klabu yake ya zamani ambayo ilimlea tangu akiwa katika kikosi cha vijana.


SOMA NA HII  DILI LA BEKI NKANA KUTUA NDANI YA YANGA LIMEVURUGWA NA MAZAWA HUYU