Home Habari za michezo SIRI YA ‘MGOLI WA CAF’ ALIOFUNGA MZIZE YAANIKWA WAZI…MCHAKATO WOTE KUMBE ULIANZA...

SIRI YA ‘MGOLI WA CAF’ ALIOFUNGA MZIZE YAANIKWA WAZI…MCHAKATO WOTE KUMBE ULIANZA HAPA..

Habari za Yanga SC

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clament Mzize amefichua siri ya bao lake lililowapeleka makundi lilitokana na maelekezo kutoka kwa kocha Miguel Angel Gamondi aliyemtaka kutumia vizuri mipira ya krosi kwa ajili ya kupachika bao na kupata ushindi.

Bao la dakika 66 lililofungwa na Mzize ndio lililowapeleka Yanga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuiondoa Al Merrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0 katika michezo yote miwili.

Nyota huyo alianzia benchi akichukuwa nafasi ya Kennedy Musonda na kufanikiwa kufunga bao pekee baada ya kuunganisha mpira wa krosi iliyopigwa na Joyce Lomalisa.

Mzize alisema akiwa katika bencho kocha (Gamond) alinipa maelekezo kuwa nikatumia vizuri mipira ya krosi na nafasi wazotengeneza ili kutafuta bao.

Alisema alienda kufanya maelekezoo aliyopewa na kufunga bao pekee ambalo amepokea krosi kutoka kwa Lomalisa na kufanya kile alichoambiwa na Gamondi.

“Aliniambia niwe makini na kutofanya makosa kwenye eneo la hatari na kutumia vizuri mipira ya krosi na nilifanikiwa kuipeleka timu hatua ya makundi.

Kuhusu kushangilia staili ya kutetema ambayo alikuwa akifanya Mayele (Fiston) kwa kuwa bado anaishi moyoni mwangu, alikuwa mtu wa kunipa moyo na hadI sasa tumekuwa tukiwasiliana na kunipa maneno ya kuweza kupambana katika hatua yangu ya uchezaji, “ alisema Mzize.

Alisisitiza kuwa hawataishia hapo hatua ya makundi kwa sababu wanahitaji kufanya vizuri katika kila mashindano na anaimani wataenda kucheza robo fainali ya Afrika kwa mwaka huu.

SOMA NA HII  SHIKALO AWACHIMBA MKWARA SIMBA