Home Habari za michezo MBRAZILI SIMBA AVUNJA UKIMYA KUHUSU WALIPOFELI MSIMU HUU…ATAJA MASTAA ‘WABOVU’…

MBRAZILI SIMBA AVUNJA UKIMYA KUHUSU WALIPOFELI MSIMU HUU…ATAJA MASTAA ‘WABOVU’…

Habari za Simba SC

Roberto Oliveira ‘Robertinho’, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizofanya wakagotea nafasi ya pili ni kuwa na wachezaji ambao hawapo fiti muda wote.

Miongoni mwa wachezaji ambao msimu wa 2022/23 ndani ya kikosi cha Simba walikuwa wanapambania hali zao ni pamoja na kiungo Peter Banda, Augustine Okrah, Moses Phiri na Aishi Manula.

Kuumia kwa Manula ambaye ni kipa namba moja wa Simba kulivuruga mwendelezo wa timu hiyo katika mataji matatu kuanzia ligi, Kombe la Azam Sports Federation na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robertinho ameweka wazi kuwa kwenye mechi zote ambazo walikuwa wanacheza kikubwa ilikuwa ni kupata matokeo lakini wakati mwingine mambo yalikuwa tofauti.

“Ilikuwa ni kupata matokeo kwenye mechi zote ambazo tulikuwa tunacheza lakini bahati mbaya haikuwa hivyo, kuna wakati wachezaji walikuwa wanasumbuliwa na majeraha hilo, lilikuwa linatufanya tusiwe na mzunguko mkubwa wa kikosi.

“Ninaamini kila mchezaji anapenda kuona tunapata matokeo hasa ukizingatia Simba ni timu kubwa na kila mchezaji anajituma kusaka matokeo kwa kilichotokea ni muda wa kujipanga kwa wakati ujao,” alisema Robertinho.

SOMA NA HII  WAZEE WA 5G LEO MZIGONI TENA....RATIBA YA MECHI ZOTE ZA MAPINDUZI CUP LEO HII HAPA...