Home Habari za michezo MGUNDA APENDEKEZA MBADALA WA MANULA SIMBA…TIMU ‘KIBAO’ ZA SAUZI ZINAMTAKA…

MGUNDA APENDEKEZA MBADALA WA MANULA SIMBA…TIMU ‘KIBAO’ ZA SAUZI ZINAMTAKA…

Tetesi za Usajili Simba

Klabu ya soka ya Simba SC imepanga kufanya Maboresho Makubwa katika Timu hiyo na eneo kubwa ambalo watafanya Maboresho kuelekea Msimu Ujao ni eneo la Golikipa, ambapo imeelezwa Kocha msaidizi Wa klabu hiyo Juma Mgunda amependekeza jina la Kipa namba Moja Wa Coastal Union na Timu ya Taifa ya Comoros Mahamoud Mroivili ambaye mkataba wake na Coastal Union unamalizika Mwishoni mwa Msimu Huu.

Tetesi zinasema kwamba kama Simba SC watapata Saini ya Mohamoud atasaini kandarasi ya Miaka Miwili.

Mbali na Simba kuhitaji Saini ya Mohamoud, Timu kadhaa kutoka Nchini Kenya na Afrika kusini zimeonesha nia ya kimhitaji mcomoro huyo.

Mpaka Sasa Mohamoud ana clean sheets 6 kwenye michezo ambayo amekaa langoni akiwa na Coastal Union Msimu Huu.

Timu ambazo amewahi kupita…

Coastal Union FC

Coffee Sport FC ya Ethiopia

Aspl 2000 Club ya Mauritius

Coin-nord Club ya kwao Comoros

Apaches Club ya Comoros

Volcan Club Comoros

Wanamsimbazi vipi Golikipa huyo?

SOMA NA HII  MIFUMO YA KOCHA MPYA SIMBA YAVUJA...BARBARA AFUNGUKA KILA KITU.. YANGA ISIFANANISHWE NA BARCELONA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here