Home Habari za michezo BAADA YA SIMBA KUMTAMBULISHA NGOMA, MASHUJAA NAO WAJIBU MAPIGO

BAADA YA SIMBA KUMTAMBULISHA NGOMA, MASHUJAA NAO WAJIBU MAPIGO

VILABU vya Mashujaa ya Kigoma na Simba ya Dar es Salaam leo vimetambulisha wachezaji wengine wapya mmoja kila timu waliojiunga na klabu hizo.

Mashujaa imemtambulisha golikipa Lukumbuzya Paschal kukipiga Lake Tanganyika msimu ujao.

“Kutoka kwenye jiji la miamba (Mwanza) Tumeinasa saini ya mkali wa milingoti mitatu Lukumbuzya Paschal kutoka klabu ya Pamba,”imesema Mashujaa.

Nayo Simba imemtambulisha kiungo mpya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

“Karibu Simba SC, Fabrice Ngoma”,imesema Simba kupitia mitandao yake ya kijamii.

Ngoma alikuwa akicheza Al Hilal ya Sudan.

SOMA NA HII  KIBU KWA SIMBA ATAKIPIGA SANA MWAMBA HUYU HAPA ATIA NENO

1 COMMENT